Vocal Fremitus
JF-Expert Member
- Oct 20, 2016
- 1,287
- 6,648
Miaka ya 2010-2012 kuna mtaa nilikua naishi. Ilikua karibu na chuo kilichopo katika makao makuu ya nchi. Kuna siku nilikua katika misele yangu njiani nikakutana na binti pisi kali haswa alinivutia sana. Alikua mdogo mdogo hivi, shape imejitenga, tumbo flat na vichuchu saa sita. Nikajiposition vizuri nikaanza kumfukuzia.
Katika stori za hapa na pale nikamuomba namba akagoma. Jibu lake ni kwamba hakua na simu, na hapendi mawasiliano na wanaume. Mkononi alishika kasimu katochi lakini akasisitiza siyo yake na hawezi kunipa namba. Kwakuwa nilikua na nia ya kuwa naye kimapenzi na njia pakee ili nikamilishe lengo langu ni kuwa na namba yake, ikabidi nimbembeleze sana anisubiri nikimbie dukani ninunue kalamu japo nimuandikie namba yangu ili akipata simu anitafute. Akakubali huku akisisitiza nifanye haraka sana. Kweli nikamuandikia namba yangu akasepa zake.
Hakuwahi kunitafuta tena. Ikawa kila nikikutana naye njiani, ananikwepa. Akipita sehem akijua nipo anajipitisha haraka haraka kwa makusudi ili nisimuite. Nikakata tamaa nikaamua kumpotezea tu mazima na kuendelea na mishe zangu. Baada ya miezi kadhaa nikaskia kuna dogo mkaanga chipsi pale mtaani anamega. Niliumia sana.
Sasa imepita miaka nane tangu nihame ile mitaa na nilishamsahau kabisa. Juzi usiku nipo kwangu nashangaa namba ngeni inanibipu. Nikapiga upande wa pili nikasikia sauti ya kike anauliza, "Wewe ndiyo Vocal Fremitus". Nikajibu ndiyo una shida gani? Akajitambulisha lakini sikuwa namkumbuka.
Baadae akanitext, kumbukumbu ikanijia. Ananiambia amenikumbuka, anatamani tuonane. Kifupi anataka niwe mpenzi wake na amejaa mazima anataka nimuoe tena bila ya mahari. Kwasasa ana watoto wawili mapacha wana miaka minne. Anadai mzazi mwenzake haeleweki na ameitelekeza familia.
Namuonea huruma. Nimemuambia amashachelewa, ingawa bado sijaoa lakini kuzaa kwake kabla ya ndoa ameshajitia doa ila anakomaa tu. Hakati tamaa. Anapiga simu zaidi ya mara 20 sipokei. Nimeblock namba. Anatumia namba ngeni kunipigia, nikianza kuskia sauti yake namblock!