Alikuwa mpenzi wangu miaka kumi ilyopita sasa anadai tuoane huku aliniacha akasepa na mzungu majuu .

Alikuwa mpenzi wangu miaka kumi ilyopita sasa anadai tuoane huku aliniacha akasepa na mzungu majuu .

Mlima Tarime

Member
Joined
Jan 27, 2012
Posts
14
Reaction score
1
Amerudi na mtoto wa kitasha ,aliniacha maskin sasa nina fedha si kama Lowasa aaa ,ya kubadilisha tu mboga yaaan tajiri wa kati nifanyeje ndugu .Ila Mtasha wake alifariki katk Vita huko Afghan
 
Duh ngoja niamngalie TV yangu inaonyesha mchele mchele
Kufia vitani Afgan na wewe ukakubali
Na licha kwamba ana mtoto bado unauliza swali ufanyeje
Na hiyo miaka kumi na wewe umekaa tuu unamsubiri
 
nenda na demu wako amuone.kwani we mlezi wa wajane?
 
Sasa labda anataka pesa zako, si wewe umeisha kuwa tajiri.
 
Ukigeuka nyuma tu utakua jiwe la chumvi,mkumbuke Luthu
 
Sijui hapa aliweka ili tumsaidie nini sasa
Au alikuwa anataka ushauri gani
 
Wewe hukuoa? Unamuhitaji huyo demu au laavl? Ana dola za kutosha ili mzungu mwingine akija asitorokee Afghanstan? But follow your heart mwisho
 
ww kubali mrudiane uende ukalambe karatasi kisha urudi umpeleke demu wako wa sasa,we unasema una hela hela yenyewe ya kibongo hii ishakuwa km zimbabwe na haichelewi kutoroka,maisha asa hivi ni mbere hapa bongo kushauzwa shauri yako,utakuja lia ww chezea zali hilo
 
Kaonane naye ila usikubali wala kukataa chochote mpaka uwe umekuja na kutueleza kama ulivyofanya ili tukushauri kwanza . haya nenda...
 
Hehehee naona unaona raha kushare na wadhungu!
 
huyu jamaa wa ajabu kweli ndio maana huyo mwanamke anamuona zoba.
kwa mwanaume wa ukweli huyo mchumia tumbo alitakiwa aona aibu hata ya kukuona lakini anajua weakness yako na si ajabu tukakukuta ukimwogesha mtoto
 
Samahani lakini ungekuwa mwanangu ningekuuliza vipi wewe khan*th*? Maana mzungu kachukuwa, kazalisha halafu katupa ndiyo wewe unakuja kuokota!

Hiyo ya Afghan haiuziki kwangu. Ana shida zake na wewe upo kwa hivyo njia rahisi ni kukudanganya.
 
Huna mwanamke wewe umekaa tu unamsubiri yeye muda wote huo?! Hawara hawaachani
 
Burudani nyumbani, hizi ndio thread za kutuchekesha chekesha kidogo maana JF hatuna music.
 
Sasa we tajiri,kwa hyo we ndo umekua mlezi wa wajane?
 
sijui unataka ushauriwe nini? Wacha ukilaza tumia akili yako. Alikuona wa kazi sasa na wewe muone wa nini?
 
Maku ziko nyingi ya kwake ina gold au? Wacha ujinga panga maisha yako na ishi utakavyo siyo ushauriwavyo. Najua moyo wako hauoni kama ni sahihi lakini unabishana na uamuzi wa nafsi ambao ni sahihi muda wote. Wacha kuwaza ujinga usinunue mizigo mingine katika maisha uliyonayo inakutosha. Kama wewe ni ******* sawa oa. LAKINI ITAKUSHINDA KWA KUWA MTOTO SI NI MDHUNGU?
 
he he, hakuondoka na mimba yako kweli?
Anaweza kuwa mtoto wako huyo
ila tu sababu ililelewa ulaya
na mtoto akatoka mlaya.
 
Back
Top Bottom