mdukuzi
JF-Expert Member
- Jan 4, 2014
- 20,925
- 51,688
Miaka kadhaa iliyopita kabla sijafulia nikiwa kwenye kilele cha ukwasi niliopoa binti mmoja mtoto mzuri sana ila mpekupeku.wale wanawake ukienda bafuni unakuta kaishasoma sms zako zote na kaishakusachi,wale ukilala anachukua kidole chako anaweka kwenye simu ili kufungua biometric password,demu kwa nje mjanja ila sikuelewa ni ushamba au,nilitoka kidogo kwenda dukani one time kurudi nakuta kapekuapekua kabatini na mabegi mlango umerudishiwa, ameshakimbia,nikampigia simu jibu alikonipa sasa!!!Mungu anabipenda kumbe wewe ni jambazi unamiliki silaha .masikini ya Mungu ile silaha naimiliki kihalali kabisa na vibali vilikuwepo ila hakuviona na upekupeku wake.