Alinisaliti, nifanyeje?



Mkuu, we endelea mbele huyo hakufai tena...inauma sana..
 
Mkuu pole sana, mjini shule, shamba kilimo!
Huyo dada hajatulia ila alikuwa akikupa ujumbe fulani ambao wewe mpaka leo hujaujua, pole sana.
1. Inawezekana kweli alitembea tena huyo mheshimiwa wakati huo wa likizo. Suala la kujiuliza ni kuwa kitu gani kilimsukuma ili atembee nae tena? Je we ulikawia kurudi toka bush? Au mzigo uliokuwa unampa haumkidhi haja ndio maana akakumbuka enzi zake?
2. Inawezekana huyo dada hakutembea na huyo jamaa, isipokuwa alikuwa anatingisha kiberiti kuku-alert uongeze ufundi na ma-care! Sio rahisi kwa hali ya kawaida mpenzi wako akwambie kuna mtu kambanjua siku za karibuni.

Mkuu nakushauri uongeze ufundi kidooooogo, uone maajabu ya dunia.
 
Last edited:
Mkuu, we endelea mbele huyo hakufai tena...inauma sana..


Mi nadhani mshauri mkuu wa swala hili ni moyo wako na feeling zako!
Je bado unampenda na anaweza kuwa mke mzuri yaani mka make it?.. songa mbele

Je humpendi?.. achana naye

Lakini kama bado unampenda nakushauri changamka uchukue kifaa mapema, kwani usipo muoa atakuja pata mwingine ukiwa unakutana naye utatamani ardhi ipasuke ujifiche.. jiulize nafsi yako unamapenzi ya kweli juu yake basi. hilo ndilo kubwa hivyo vijisabau vingine kwangu naona ni vya kitoto!
Watu wanawafumania wake/waume wa ndoa kabisa wana sameheana na bado wanaishi, sembuse boyfriend tena kakwambia mwenyewe? na je unge wakutiliza akiwa anakuficha?

Uamzi ni wako bro!
 

...chukua karatasi, chora msitari katikati, upande wa kushoto andika mabaya yake, upande wa kulia andika mazuri yake... linganisha kati ya mabaya na mazuri yepi yalozidi mwenzie,..kisha ichane hiyo karatasi kisha amua uachane nae kwa mabaya yake au uendelee nae kwa mazuri yake.

unasex nae na condom cku zote. leo anakuja kukwambia ana mimba na alishakutana na huyo ex wake hapo kati ukiwa haupo, kuna cku condom ilipasuka?....kuna walakini hapo bro!

...kama soksi vile,

inategemeana na uvaaji na uvuaji nyamayao. Halafu kuna wale wanaotumia size kubwa kuliko 'mguu' wao, huchelewi ikuta ishavuka ipo kwenye unyayo,... akipitiwa na kale kausingizi baada ya kuuona wavu ndio kabisaaaa 'inamvuka!'
 
Move on mkuu!..Sikiliza wimbo wa broken strings utanielewa vizuri!...Usipende kupata presha ilhali bado ni kijana na muda+nafasi unayo kuwa na mwingine, focus kwa career yako na ishalaah Mola atakusaidia upate mpenzi tena.
 
Move on mkuu!..Sikiliza wimbo wa broken strings utanielewa vizuri!...Usipende kupata presha ilhali bado ni kijana na muda+nafasi unayo kuwa na mwingine, focus kwa career yako na ishalaah Mola atakusaidia upate mpenzi tena.

...😀 te he, BJ tatizi sio ku move, ...tatizo ni ku move forward hatua ya kwanza, kisha ya pili na ya tatu bila (temptation za) kugeuka nyuma! wengi ndio wanapofeli hapo!
 

Nashukuru kwa ushauri wako senior, zinaweza kuwa sababu za kitoto kwa mtazamo wa watu wengine ila kwangu zikawa na uzito. By the way thanks alot
 
Move on mkuu!..Sikiliza wimbo wa broken strings utanielewa vizuri!...Usipende kupata presha ilhali bado ni kijana na muda+nafasi unayo kuwa na mwingine, focus kwa career yako na ishalaah Mola atakusaidia upate mpenzi tena.

Asante sana. Unajua mapenzi kweli husipoyajua ni presha iliyo na kifo cha ghafla sana. Ila namuomba Mungu sana anipe nguvu ya kutatua jambo ili kusema kweli linaniumiza sana kwasababu i want to go forward na maisha ya mbele lakini sina amani moyoni.
 

Bwana Mbu kusema kweli dhana niliyokuwa navaa ilikuwa inanikaa fresh sana na hakuna siku ambayo iliwahi kuvuka wala kupasuka. Nilikuwa makini sana. Ndio maana aliponiambia ana mimba nilishtuka sana nikamuuliza ananitania au yuko seriuos. Mpaka akaenda hospitali. Ilinichanganya sana kwa sababu nilitegemea mwenzangu angeniambia kuwa nilikuwa nakutania. Sijui kama kweli alikuwa na mimba akatoa au la. Yeye ndio anajua ukweli
 
unasex nae na condom cku zote. leo anakuja kukwambia ana mimba na alishakutana na huyo ex wake hapo kati ukiwa haupo, kuna cku condom ilipasuka?....kuna walakini hapo bro!

Dada Nyamao hakuna siku condom iliwaji kupasuka wala kujivuka. Ilikuwa mechi inaisha salama. Ndio maana siku aliponiambia kuwa anahisi kuwa na mimba nilishtuka na kushangaa sana. Nashukuru kwa ushauri dada
 

Nashukuru sana Idea, kusema kweli huyu binti ananipenda lakini ni baada ya kuona niko serious na maisha kuliko alivyofikiri hapo mwanzoni. Hadi kwao nilishafika lakini sio kama mchumba ila nilienda kama rafiki wa chuo tu. Ila baadhi ya dada na kaka hata wadogo zake wanafahamu kuwa tu wapenzi. Ila toka aliponichefua kidogo nilikata mawasiliano. Kusema kweli hata zawadi alikuwa ananinunulia sana tofauti na mimi. Lakini mimi naona yote ilikuwa katika kuniziba macho ili nisione kinachoendelea. Nasema hivyo kwa sababu kuna kipindi kuna mshikaji alikuwa anamtokea siku moja nikamuuliza kwa nini fulani anakufuata sana akaniambia na yeye si anataka. Mmmh! nilishtuka.
 
Wana JF bado naendelea kupokea ushauri wenu kwa makini naamini sehemu kubwa ya uamuzi wangu nitakaouchukua utachangiwa na maoni kutoka kwenu. Napenda kuwashukuru wote walionishauri, siwezi kumtaja mmoja mmoja kwani ni wengi sana mmenishauri. Naua ni heshima kubwa sana mtu kupoteza muda na kuandika paragraph moja kumsahuri kwaajili ya maisha yake na familia yake. Ila niweke wazi tu MAPENZI hayana Senior, Junior, Expert wala Premium. Ni suala la kumoumba MUNGU tu tupate wake na waume wenye hekima ili tuepuke mwisho mbaya. Asanteni sana
 
Asante sana. Unajua mapenzi kweli husipoyajua ni presha iliyo na kifo cha ghafla sana. Ila namuomba Mungu sana anipe nguvu ya kutatua jambo ili kusema kweli linaniumiza sana kwasababu i want to go forward na maisha ya mbele lakini sina amani moyoni.

...inasikitisha lakini ndio hivyo tena, inabidi uchukue maamuzi mazito na magumu. Inaonekana ni kweli umeshaamua kusonga mbele ila tatizo ni MAZOEA yanakupa tabu.

...umejenga mazoea gani na huyo mrembo? kupigiana simu? kutembeleana? kuwa pamoja kila wikiendi? nk? ...well, huu ni mtihani tu wa maisha, njia rahisi ya kuanzia ni kupunguza yale mazoea yaliyo nje ya uwezo wako mfano; kusalimiana nae, kupokea simu zake ...na kuyaacha yaliyo ndani ya uwezo wako i.e kujaamiana nae, kumpigia simu, kumfuatilia maisha yake, nk...

Kubwa kuliko yote, hayatawezekana haya bila wewe kumwambia ukweli wako kuwa yeye na wewe sasa basi!
 
Anakwambia katembea na ex-BF wake juzi juzi tu, mara ana mimba wakati anajua unajua mlikuwa mnatumia condoms kila wakati wa tendo......na wewe bado unashangaa tu? Ama kweli penzi humtia mtu upofu. Ulipaswa kupiga chini long time bro...

Kwa nini uliendelea nae mpaka leo? By the way, umemaliza chuo lini?
 
Sipo mke mwema hutoka kwa Bwana, na apataye mke amepata kitu chema.
 
Dada Nyamao hakuna siku condom iliwaji kupasuka wala kujivuka. Ilikuwa mechi inaisha salama. Ndio maana siku aliponiambia kuwa anahisi kuwa na mimba nilishtuka na kushangaa sana. Nashukuru kwa ushauri dada



kaka unasubiri nini tena?
 
Sipo mke mwema hutoka kwa Bwana, na apataye mke amepata kitu chema.

dada Pretty, ni kweli mke mwema anatoka kwa MUNGU, lakini sijajua unachomaanisha hapa ni nini hasa. please endelea kunidadafulia
 

Sinyolita kama ulivyosema mapenzi humtia mtu upofu ndio maana nipo hadi leo lakini kwa kusita sita
 
Kwani kaka tangu alipokutana na huyo ex na wewe ulivyoreact baada ya kukwambia ameshafanya kitu kama hicho tena? Je kuna kingine ambacho kinaweza kuwa kimeashiria kutokuwa muaminifu?

Kwanza mimi ninaamini kabisa mpaka akwambie wewe ukweli kuwa nilikutana na ex wangu juzi huyu ni mwaminifu sana kwako kwa sababu angeweza kukwambia kuwa hajakutana naye miaka wala hajui alipo. Kaka wanawake huwa tuna tabia ya kupenda kuonekana wasafi so kwa kitendo hicho nampa pongezi wifi kwa kuwa mkweli kwako.

Chunguza kama hakutani naye tena na wala hana dalili ya kutokuwa muaminifu kwako. Kama kosa hilo la kukwambia ukweli ndio doa pekee, please think twice before dumping her kwa kosa hilo
 
kaka unasubiri nini tena?

dada Nyamao, ushauri wenu umenifaa sana, unajua unapokuwa na mpenzi unaweza kuona ukimuacha huyo umpati wa kufanana naye lakini siku zinavyokwenda na-realize kuwa nilikuwa na mawazo mgando. thanks in advance
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…