EL ELYON
JF-Expert Member
- Jan 2, 2013
- 1,565
- 1,918
Wakuu mmebarikiwa Sana na MUNGU WA MBINGUNI.
Imepita miaka sasa niliwahi kuishi na mwanamke mmoja muha mwanamke jeuri, matusi, kiburi, uchafu, ujuaji sijampata ona, harakati ndani ya familia, kutaka kunitawala. Nilipohitimu chuo niliamua kuanza maisha yaani niliondoka home kabisa nikaanza maisha nikiwa nimefungua Duka lengo likiwa nisikose pesa za kusogeza siku nikiwa napambana.
Kunal binti nilikuwa na mahusiano Naye toka mwaka WA pili Naye alisema hawezi Rudi home kwao huko mkoani kwani anaishi na mama yake ni mkorofi Sana kwahiyo Bora tuishi wote Tu yeye ataongea naye kwamba Yuko wapi. Nikamwambia sawa kweli maisha yalianza ye akiwa kasomea ualimua Mimi Mambo uongozi. Shughuri ilianza pale zilipotoka kazi si mnajua Enzi za kikwete walimu walikuwa wanaajiriwa wote Tu na mnajaza vituo vya kazi mara mnapohitimu chuo.
Alifanikiwa kupata kazi mkoa tuliokuwepo DSM sasa nikasema afadhari imetupunguzia ukali WA maisha kumbe nilikuwa najidanganya. Wakati huo tulikuwa na mtoto wetu binti akiwa na miaka mitatu na miezi kadhaa. Siku zilisonga Mimi nikiwa nachapa zangu kazi KWENYE Duka nililofungua pale center kitaa huku naangalia uwezekano WA kupata ajira.
Siku zilisonga nikaanza kuona mabadiliko ya mwenzangu ndani kiburi mara ARUDI usku mara majibu ya mkato mara agome kupika, yaani shughuri hasa sjui huko alikuwa anakwenda kazini wenzie walikuwa wanamdanganya hata sielewi. Akapata ujauzito WA pili tukalea mimba akajifungua salama mtoto WA kiume sasa mtoto alipoanza kupata nguvu akiwa kama na miezi miwili na siku kadhaa kimbembe kikaanza yaani sasa Moto ukawaka Zaid najua Kunal wengine watasema sikuwa na hela au nilikuwa nalishwa na mwanamke si kweli kupitia Duka langu nilikuwa nasomesha mtoto wangu shule ya kulipia nursery nalipa Ada takriban laki 5 Kodi ya nyumba nalipa mwenyewe zaidi Naye alikuwa anasaidia kiasi Fulani. Mtaji wa Duka wote ulikuwa wangu.
Siku moja aliamka asubuhi kwenda kazini kwake akajiandaa kulikuwa na Dada WA kazi aliyekuwa anakuja kubaki na mtoto angalau mpaka Sana SITA mchana na mama MTU akirudi binti anaondoka. Sasa siku hiyo mama mtoto aliondoka tena tukaagana vizuri Tu akaenda kazini nashanga mpka inafika Sana nne usku kimya simu haipatikani mtoto ameshasumbua hatari Sana, mpaka saa Saba usiku kimya nikaamua kulala Tu maana sikuwa na namna.
Siku ya pili tena mpaka inafika saa tano asubuhi kimya, nikampgia simu mama yake kumpa taarifa kisha nikaanza tafuta mawasiliano ya huko shuleni kwake kujua kama anafika mkumbuke hapo Nina kichanga cha miezi miwili Tu. Nilifanikiwa kupata namba ya mkuu WA shule nikampa taarifa kuhusu mfanyakazi wake simuoni nyumbani na kuna mtoto WA miezi miwili hapa je kazini anafika?
Yule MKuu Wa shule akasema niende shuleni mmmh nikasema Acha niende, nilifika nikapeleka ofisini ndani mkuu WA shule na msaidizi wake tulzungumza nikawapa Hali halisi lakini wakasema hawajamuona hapo shuleni nikawaaga nikaondoka. Jioni Yule mkuu WA shule akanipigia simu kwamba kweli mwl wake alikuwepo Ila alimwambia ajifiche kwani uwenda ningemuona ningelianzisha pale kwahiyo kesho yake niende tena shuleni nikamwambia sifanyi biashara hiyo akumbuke kaacha mtoto wa miezi miwili hapa kama hataki kurudi nyumbani akae hukohuko.
Siku ya nne usiku saa Saba nasikia mlango unagongwa kuna Jamaa tangu tulikuwa tunasali Naye akaomba nifungue nikafungua nikamkuta Yuko na wamama wawili na Dada niliyekuwa naishi Naye pamoja na mjumbe WA mtaa wakanisihi nitoke tuzungumze nikatoka eeeh ikaanza kesi mi nikawaambia sina cha kuzungumza Ila kama huyu aliyekimbia mtoto anacho cha kusema na aseme akaongea pale hata vitu haieleweki mpaka mama mmoja waliyekuwa Naye akataka kumpiga.
Kiukweli sitasahau vile mtoto wangu aliteseka na alishafariki Kwa upungufu WA Damu sickle cell ilimpata. Ila alikuwa ameshakuwa mkubwa WA mwaka kama na nusu. Na Mama ake tulishaachana Kila Mtu na maisha yake Ila mtoto wangu WA Kwanza alisema mpka nimkate shingo ndo atanipa mtoto so nilimuachia.
Haya ndo maisha wakuu Ila mpaka Leo Yule mtoto ananiuma Sana aliyetangulia mbele za haki.