Alipata kuandika Thadei Ole Mushi, mwaka 2018. Makala ya kusisimua, inayoishi

Alipata kuandika Thadei Ole Mushi, mwaka 2018. Makala ya kusisimua, inayoishi

TAJIRI MKUU WA MATAJIRI

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2010
Posts
11,999
Reaction score
24,328
TAALUMA HII YA KIJASUSI IMEKWENDA WAPI?

Na Thadei Ole Mushi.

#Spin Doctor ni taaluma ya kijasusi ya kubadili hali ya mambo. Taaluma hii hutumiwa sana sana na wanasisa katika kuondoa mijadala na kashfa kubwa zinazowakumba.

#Hizi picha zilipigwa mwaka 2008 ni miaka 10 sasa toka kundi la waliojiita WASABATO MASALIA walipotaka kusafiri kwenda Ulaya bila kuwa na nauli wala Passport na Visa.

#Ni kundi lililoibuka gafla na kupata umaarufu mkubwa. Kundi hili ndilo lililofanikiwa kuondoa mjadala wa Richmond mtaani. Ulikuwa ni mwaka huo huo ambao Mh Edward Lowassa alijiuzulu. Mjadala wa Richmond ulikuwa kwenye media kila siku, ujio wa wasabato masalia uliuondoa mjadala kwenye media wakabakia Mwanahalis tu wakikomaa nao.

#ESCROW:- Hii ni Kashfa ya pili kubwa kuikumba Serikali ya JK, kabla ya Kashfa hii Rais alijiweka kwenye mazingira ya kuonewa huruma. Wakati mjadala wa Escrow unaanza kujadiliwa Bungeni Rais Kikwete alisafiri kwenda Marekani kutibiwa.

#Matibabu yake yaliwekwa wazi kabisa kiasi kwamba watu waligawanyika wengine waliamua kufuatilia ugonjwa mpya ambao haukuwa maarufu sana nchini wa TEZI DUME wengine sakata la Escrow. Kila kitu kilikuwa kinaripotiwa toka marekani. Rais naye alishiriki kuukuza mjadala kwa kuelezea hali yake inaendeleaje.

#Siku ya Kurudi alipokelewa Uwanja a Ndege kama kiongozi mwenye mvuto mkubwa sana, baada ya muda kama wiki akaitisha Press kwa sauti laini kabisa kina Tibaijuka wakapigwa chini na mjadala ukaisha.....

#Clinton na Scandal ya Monica Lewinsky, Wakati Clinton akiwa madarakani Chama cha upinzani kwa kipindi hicho cha Republican kiliibua kashfa kubwa aliyoifanya Bill Clinton ya kufanya mapenzi na binti aliyekuwa anafanya field ikulu ya Marekani (Monica Lewinisky)

#Kashfa ile si kwamba ilitikisa nafasi yake tu ya urais bali ilitikisa ndoa yake kidogo ivunjike. Taaluma hii ya Spin ndio iliyomuokoa na kubaki salama. Timu iliundwa na kazi kubwa ilikuwa ni kutofautisha Bili Clinton kama binadamu na raia wa kawaida na Bill Clinton kama Rais wa marekani.

#Ni katika kipindi hicho vilichapwa vitabu na majarida Mengi sana ya kuelezea ni kwa namna gani Clinton amefanikiwa katika swala la Uchumi wa marekani. Timu hii ilifanikiwa kuteka Media karibia zote. Mwisho kabisa Timu hii ikamwambia kumaliza mchezo ajitokeze hadharani kuomba msamaha familia yake na taifa zima la marekani.

#Pamoja na Kashfa hiyo Clintoni aliondoka ikulu huku Image yake ikiwa na mvuto ule ule.

#Obama na uchaguzi wa kurudi Ikulu kipindi cha pili. Kama Obama hakuzichanga karata zake vizuri Ikulu angelikaa kwa kipindi kimoja tu. Kwa kulijua hilo Obama alijikita kuhakikisha amewateka wamarekani. Tukio la Kumuua Osama Bin Laden lilikuwa karibu sana na Uchaguzi. Wamarekani kwa kusikia tukio hilo walipagawa mno na kufanya sherehe.

#Hakuna mtu aliyewahi kuona Mwili wa Osama wala kaburi lake wanadai walimzika Baharini....... akili kubwa sana hii.

#Trump anataka kumaliza kashfa yake ya kufanya ngono na kahaba kabla ya kuwa rais kwa kufanya kitu ambacho wengi hawakutarajia kufanywa na rais wa marekani. Ziara ya Trump kwenda kumuona rais wa Korea Kaskazini ina sura na taswira ya spin doctor.

Taaluma hii inatakiwa kuandaliwa na watu wenye uwezo mkubwa wa kutafsiri mambo. Mashirika ya kijasusi huwa ndio kiini cha mipango yote ila wanaweza kuwatumia watu walio njee ya mfumo ili kuficha hali halisi.

Kwa sasa taaluma hii haiandaliwi ikaiva hivyo inapokuja kurekebisha hali ya mambo watu hungamua badala ya kuondoka kwenye mjadala huzidisha mjadala, matokeo yake ni kutumia nguvu kuzima mjadala.

Ole Mushi
 
Back
Top Bottom