Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
ALIPOTOKA MAALIM HADI KUFIKA HAPA
Uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi mwaka wa 1995 ulijaa hamasa nyingi kwa chama cha CUF kwa namna ya pekee hasa Zanzibar.
Nimeeleza hapa nini kilitokea baada ya kupiga kura na ZEC kushindwa kutoa matokeo ya kura ya Rais kwa muda uliotakiwa na sababu ya kushindwa kutoa matokeo inasemekana ni kuwa Salimin Amour alikuwa ameshindwa na Maalim Seif katika uchaguzi wa Rais wa Zanzibar.
Nilikuwapo Zanzibar na niliiona hali ya unyonge iliyowagubika CCM.
Halikadhalika niliona sura za matumaini na furaha walizokuwanayo wafuasi wa CUF kwa kusikia zile tetesi kuwa Maalim kashinda kura ya Rais.
Binafsi niliamini kuwa Maalim Seif ameshinda kwani nilikuwa najiambia kwa nini ZEC ichelewe katika majumuisho ya kura chache tu?
Niliamini kama wengi walivyoamini na hawa pamoja na wafuasi wa CCM kuwa ingekuwa CCM imeshinda matokeo yangetagazwa mapema na shamrashamra za kushangilia ushindi zingekuwa tayari zimeanza.
Tukawa tunasubiri matokeo kutoka ZEC na usiku unakuwa mrefu sana kama vile hakutokucha.
Baada ya uchaguzi ule nikawa sina wasiwasi hata tone kuwa CCM Zanzibar haitaweza kamwe na narudia haitaweza kamwe kushinda uchaguzi Zanzibar.
Huu ulikuwa ndiyo utabiri niliofanya miaka 25 iliyopita.
Na sikukosea utabiri umesimama pale pale.
Kila uchaguzi ni matatizo makubwa.
Nilijiuliza vipi CCM Zanzibar juu ya kuwa katika uongozi toka mwaka wa 1964 imeshindwa na chama kichanga chenye umri wa miaka 3?
Nikahama katika swali hili nikaja kuangalia picha kubwa zaidi kutaka kuchambua nini maana ya ushindi wa CUF na nini maana ya kushindwa kwa CCM?
Hapa nikawa nimejitisha mimi mwenyewe natamani muda wote nitembee kwenye kiza ili nisikione kivuli change nyuma kinanifuata.
Sikutaka taa zizimike ili ninusirike na hofu iliyokuwa inaletwa na kivuli changu.
Kushindwa kwa CCM maana yake ni kuwa Wazanzibari wameyakataa mapinduzi ambayo yalikuwa yemongezewa vibwagizo viwili.
Mapinduzi Matukufu na Mapinduzi Daima.
Uchaguzi wa mwaka wa 1995 uliiingiza katika fikra za viongozi wa CCM Zanzibar na Bara kuwa Wazanzibari wamekanyaga kwa viatu vyao kile ambacho kilikuwa kikielezwa kuwa ni kitukufu na Wazanzibari wamekata mshipa uliokuwa unapitisha damu ya uhai wa Mapinduzi.
Mapinduzi kumbe hayakuwa na uhai wa kudumu daima.
Maalim Seif hakuwa kiongozi wa kuchezewa ameyaangusha mapinduzi muasisi wa mapinduzi akiwa yu hai na anapumua.
Ikiwa mapinduzi yamesiginwa na Wazanzibari nini itakuwa hali ya muungano?
Maalim akitaka anaweza kuvunja Muungano au kufanya marekebisho makubwa ya Muungano?
Hizi ndizo fikra zilizokuwa zikipita katika vichwa vya viongozi wa CCM.
Kishindo alichozua Maalim hakisemeki.
Maneno ni mengi kiasi nashindwa kutambua lipi la kweli lipi ni porojo za kustawisha barza.
Mpashaji wangu anasema, ‘’Mwalimu Nyerere alipata mshtuko mkubwa.’’
Mwalimu alijilaumu akaona kama vile amemwachia Komando akaliwe na simba Maalim bila ya kumtayarisha sawasawa.
Haraka sana katika siku zile za kusibiri matokeo ya uchaguzi wa rais Zanzibar alihangaika vipi amnusuru Salmin Amour kama kiongozi, ainusuru CCM Zanzibar, ayanusuru Mapinduzi na ‘’typical’’ yaani kama alivyokuwa Baba wa Taifa ajinusuru yeye mwenyewe.
Nyerere akijali sana heshima yake vipi dunia itakavyomwangalia.
Maalim alikuwa amemchukua Nyerere, Waingereza wanasema, ‘’head on,’’ yaani kapambana na Nyerere uso kwa uso bila ya kupepesa na kampiga mwereka.
Maalim alikuwa ameshinda vita askari wake wakipigana katika ‘front’’ zote na kote walikuwa wanaelekea kupata ushindi.
Wazanzibari walikuwa wameamua.
Wenzetu wana msemo wanoutumia katika uchaguzi matokeo yanapotoka.
‘’The people have spoken.’’
In Shaa Allah itaendelea…
Maalim...