Alipotoka Maalim Seif hadi kufika hapa

Alipotoka Maalim Seif hadi kufika hapa

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
ALIPOTOKA MAALIM HADI KUFIKA HAPA

Uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi mwaka wa 1995 ulijaa hamasa nyingi kwa chama cha CUF kwa namna ya pekee hasa Zanzibar.

Nimeeleza hapa nini kilitokea baada ya kupiga kura na ZEC kushindwa kutoa matokeo ya kura ya Rais kwa muda uliotakiwa na sababu ya kushindwa kutoa matokeo inasemekana ni kuwa Salimin Amour alikuwa ameshindwa na Maalim Seif katika uchaguzi wa Rais wa Zanzibar.

Nilikuwapo Zanzibar na niliiona hali ya unyonge iliyowagubika CCM.

Halikadhalika niliona sura za matumaini na furaha walizokuwanayo wafuasi wa CUF kwa kusikia zile tetesi kuwa Maalim kashinda kura ya Rais.

Binafsi niliamini kuwa Maalim Seif ameshinda kwani nilikuwa najiambia kwa nini ZEC ichelewe katika majumuisho ya kura chache tu?

Niliamini kama wengi walivyoamini na hawa pamoja na wafuasi wa CCM kuwa ingekuwa CCM imeshinda matokeo yangetagazwa mapema na shamrashamra za kushangilia ushindi zingekuwa tayari zimeanza.

Tukawa tunasubiri matokeo kutoka ZEC na usiku unakuwa mrefu sana kama vile hakutokucha.

Baada ya uchaguzi ule nikawa sina wasiwasi hata tone kuwa CCM Zanzibar haitaweza kamwe na narudia haitaweza kamwe kushinda uchaguzi Zanzibar.

Huu ulikuwa ndiyo utabiri niliofanya miaka 25 iliyopita.

Na sikukosea utabiri umesimama pale pale.

Kila uchaguzi ni matatizo makubwa.

Nilijiuliza vipi CCM Zanzibar juu ya kuwa katika uongozi toka mwaka wa 1964 imeshindwa na chama kichanga chenye umri wa miaka 3?

Nikahama katika swali hili nikaja kuangalia picha kubwa zaidi kutaka kuchambua nini maana ya ushindi wa CUF na nini maana ya kushindwa kwa CCM?

Hapa nikawa nimejitisha mimi mwenyewe natamani muda wote nitembee kwenye kiza ili nisikione kivuli change nyuma kinanifuata.

Sikutaka taa zizimike ili ninusirike na hofu iliyokuwa inaletwa na kivuli changu.

Kushindwa kwa CCM maana yake ni kuwa Wazanzibari wameyakataa mapinduzi ambayo yalikuwa yemongezewa vibwagizo viwili.

Mapinduzi Matukufu na Mapinduzi Daima.

Uchaguzi wa mwaka wa 1995 uliiingiza katika fikra za viongozi wa CCM Zanzibar na Bara kuwa Wazanzibari wamekanyaga kwa viatu vyao kile ambacho kilikuwa kikielezwa kuwa ni kitukufu na Wazanzibari wamekata mshipa uliokuwa unapitisha damu ya uhai wa Mapinduzi.

Mapinduzi kumbe hayakuwa na uhai wa kudumu daima.

Maalim Seif hakuwa kiongozi wa kuchezewa ameyaangusha mapinduzi muasisi wa mapinduzi akiwa yu hai na anapumua.

Ikiwa mapinduzi yamesiginwa na Wazanzibari nini itakuwa hali ya muungano?

Maalim akitaka anaweza kuvunja Muungano au kufanya marekebisho makubwa ya Muungano?

Hizi ndizo fikra zilizokuwa zikipita katika vichwa vya viongozi wa CCM.

Kishindo alichozua Maalim hakisemeki.

Maneno ni mengi kiasi nashindwa kutambua lipi la kweli lipi ni porojo za kustawisha barza.

Mpashaji wangu anasema, ‘’Mwalimu Nyerere alipata mshtuko mkubwa.’’

Mwalimu alijilaumu akaona kama vile amemwachia Komando akaliwe na simba Maalim bila ya kumtayarisha sawasawa.

Haraka sana katika siku zile za kusibiri matokeo ya uchaguzi wa rais Zanzibar alihangaika vipi amnusuru Salmin Amour kama kiongozi, ainusuru CCM Zanzibar, ayanusuru Mapinduzi na ‘’typical’’ yaani kama alivyokuwa Baba wa Taifa ajinusuru yeye mwenyewe.

Nyerere akijali sana heshima yake vipi dunia itakavyomwangalia.

Maalim alikuwa amemchukua Nyerere, Waingereza wanasema, ‘’head on,’’ yaani kapambana na Nyerere uso kwa uso bila ya kupepesa na kampiga mwereka.

Maalim alikuwa ameshinda vita askari wake wakipigana katika ‘front’’ zote na kote walikuwa wanaelekea kupata ushindi.

Wazanzibari walikuwa wameamua.

Wenzetu wana msemo wanoutumia katika uchaguzi matokeo yanapotoka.

‘’The people have spoken.’’

In Shaa Allah itaendelea…

Maalim...
Screenshot_20201122-205144.jpg
 
Maalim Mohamed, kuna hadithi za siku nyingi kwamba Maalim Seif ndiye alimuuza marehemu Aboud Jumbe kwa Nyerere baada ya kuichukua document muhimu ambayo Jumbe akiiandaa kuhusiana na mustakabali wa aina ya Muungano waliokua wanaitaka Wazanzibari na alipokwenda na Jumbe alipokwenda kwenye vikao vya CCM Dpdoma akakuta na nyaraka ile ikiwa mikononi mwa Mwalim Nyerere.

Je unaweza kututhibitishia hili? Na kama ni kweli Je, Maalim Seif atakua na moral authority ya kudai muundo wa muungano wa serikali tatu na mamlaka kamili ya Zanzibar ilhali alishatanguliza kufanya khiyana kwa Mzanzibari mwenzie aliyekua akipigania jambo hilohilo?
 
Maalim Mohamed, kuna hadithi za siku nyingi kwamba Maalim Seif ndiye alimuuza marehemu Aboud Jumbe kwa Nyerere baada ya kuichukua document muhimu ambayo Jumbe akiiandaa kuhusiana na mustakabali wa aina ya Muungano waliokua wanaitaka Wazanzibari na alipokwenda na Jumbe alipokwenda kwenye vikao vya CCM Dpdoma akakuta na nyaraka ile ikiwa mikononi mwa Mwalim Nyerere.

Je unaweza kututhibitishia hili? Na kama ni kweli Je, Maalim Seif atakua na moral authority ya kudai muundo wa muungano wa serikali tatu na mamlaka kamili ya Zanzibar ilhali alishatanguliza kufanya khiyana kwa Mzanzibari mwenzie aliyekua akipigania jambo hilohilo?
Umeniwahi mkuu...

Nilikuwa nataka kuuliza hili swali

Mohamed Said tusaidie hapa
 
Umeniwahi mkuu...

Nilikuwa nataka kuuliza hili swali

Mohamed Said tusaidie hapa
Mtama...

Siku moja Mzee Jumbe alitupa kisa cha, ‘’The Long Letter.’’

Hii barua ndefu ilikuwa ile barua iliyotayarishwa na Bashir Swanzy Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar ndani yake yakiwa mashtaka dhidi ya Muungano kuhoji uhalali wa wa Muungano.

Barua hii ilikuwa imekusudiwa iwasilishwe kwenye Mahakama Maalum ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

Mzee Jumbe alikuwa akitualika mara kwa mara nyumbani kwake na yeye akipenda sana kuandalia.

Mzee Jumbe akikualika nyumbani kwake kula, inabidi ujitayarishe vyema kwani alikuwa akichafua uwanja.

Ilikuwa katika moja ya barza zetu kama hizi ndipo siku hiyo akatuhadithia yale yaliyotokea Dodoma kati yake na Nyerere kupelekea yeye kujiuzulu nyadhifa zake zote.

Mzee Jumbe alikuwa ana namna ya kuhadithia jambo hata liwe zito vipi, wewe msikilizaji likakufikia kwa wepesi na wakati mwingine katika njia ya kukufanya ucheke.

Alikuwa keshatuhadithia jinsi mashtaka yale yalivyokuwa yametayarishwa na hapo ndipo alipokuja na jina hilo la, ‘’The Long Letter,’’ na sisi ikawa huo waraka tunauita, ‘’Long Letter,’’ kama yeye mwenyewe, katika njia ya utani alivyopenda kuita.

Mzee Jumbe alipokuwa anaeleza kupotea kwa waraka ule na ukaibuka mikononi kwa Nyerere Dodoma, Mzee Jumbe alikuwa akituchekesha alivyokuwa akitueleza jinsi Nyerere alivyoinga’nga’nia, ‘’The Long Letter,’’ na akawa anasoma vipande alivyovipenda yeye na Jumbe akimwambia endelea na soma na mahali pengine, Nyerere alivyokuwa hataki akishikilia hapo hapo kama mtoto mdogo aliyepewa pipi na sasa anahisi anataka kunyang’ang’anywa.

Huku tukishusha biryani na juisi baridi, hakika ilikuwa ni burdani ya aina yake. Mzee Jumbe akicheka na sisi wasikilizaji tukicheka pia.

Mzee Jumbe Uislam na kukubali qadar ya Allah kulikuwa kumemweka pazuri sana.

Mzee Jumbe hakuwa mtu aliyejuta kutoka katika uongozi kiasi alikuwa sasa anatushekesha kuhusu madhila ya uongozi.

Akawa siku zote tukiizungumza na yeye kuhusu, ‘’The Long Letter,’’ masikitiko yake ni kuwa kuikosa, ‘’The Long Letter,’’ hawezi kuandika kitabu kuhusu matatizo ya Muungano.

Siku zikenda na miaka ikapita.

Siku moja tuko kwake akatuangushia bomu lililotuacha midomo wazi.

Mzee Jumbe akatuambia kuwa, ‘’The Long Letter,’’ kaiona nyumbani kwake Migombani kwenye, ‘’Study Room,’’ yake.

Tulimuuliza Mzee Jumbe kaiona vipi?
Yeye akatujibu kuwa na yeye amepigwa na mshangao kama tulivyopigwa sisi.

Akatuambia kuwa na keshaanza kuandika kitabu.

Siku zile Mzee Jumbe tayari alikuwa keshaanza kupoteza nuru ya macho na akiandika na kusoma kwa msaada wa ‘’lens.’’

Iko siku mimi na mwenzangu sasa tukihariri mswada wa kitabu cha Mzee Jumbe kilichokuja kujulikana kama, ‘’The Partner-ship: Tanganyika-Zanzibar Union 30 Turbulent Years.’’

Mzee Jumbe alitualika nyumbani kwake Zanzibar Migombani na tulisafiri meli moja.

Siku ile alituingiza katika ‘’Study Room,’’ yake na akatuonyesha ‘’desk,’’ alipoikuta, ‘’The Long Letter,’’ikimsubiri, imerejeshwa kama ilivyoibiwa ofsini kwake Ikulu Zanzibar.

Kwangu mimi binafsi ilikuwa furaha ya pekee.

Nakumbuka wakati tumekaa tunajiuliza ni nani aliyeirudisha, ‘’The Long Letter,’’ nyumbani kwa Mzee Jumbe na asionekane na mtu.

Hakika kilikuwa kitendawili.

Mzee Jumbe alikuwa mtu wa kupenda kuandalia chakula kama nilivyosema hapo awali.

Wakati sote tumeinamisha vichwa tunamsikiliza jinsi alivyoiona, ‘’The Long Letter,'' ghafla wakaingia watu wa ‘’catering,’’ na mavazi yao meupe wamebeba sahani za vyakula wanatuandalia.

Ilikuwa kiasi cha saa kumi na moja jioni.

Kile ambacho Aboud Jumbe hakupewa nafasi kukisema Dodoma Allah akamuwezesha kukisema miaka 10 baadae kupitia kitabu chake, ‘’The Partner-ship: Tanganyika-Zanzibar Union 30 Turbulent Years.’’

Mzee Jumbe alikuwa mtu wa vichekesho sana.

Tulikuwa tunachagua picha za kitabu sasa tukawa tunaangalia picha moja Karume na Nyerere wamepanda gari la wazi.

Mmoja wetu akamuuliza Mzee Jumbe, ‘’Hii picha tuweke, ‘’caption gani?’’ Mzee Jumbe mara moja hapo kwa hapo akajibu, ‘’Karume being taken for a ride by Nyerere.’’ Sote tuliangua kicheko.

Nadhani hapa tulipofika panatosha.
Huwezi mtu ukammaliza Mzee Jumbe.

Nina mengi ningeweza kueleza kuhusu Aboud Jumbe na juhudi zake za kuwasaidia Waislam khasa wa Bara.

Mzee Jumbe alikuwa karibu sana na viongozi wa Waislam Bara na alijitahidi sana kuwasaidia kwa hali na mali akifanya mambo yake kimya kimya. Darul Iman walipofanyiwa hujuma wasijenge shule ya ufundi Kibaha.

Darul Iman walifunga virago na fedha zile wakataka kuzipeleka Somalia.

Mzee Jumbe hakukubali aliwaambia kuwa ikiwa watafanya hivyo watakuwa wamewadhulumu Waislam wa Tanzania kwani hizo fedha zimetolewa kwao.

Mzee Jumbe akawaambia kuwa Tanzania ni nchi mbili, ikiwa bara Waislam wanazuiliwa kujengewa hiyo shule hizo fedha zipelekwe Zanzibar na yeye atahakikisha kuwa ardhi inapatikana na shule inajengwa.

Mzee Jumbe alipotuambia kuwa kanifanikiwa kuzirejesha fedha za Darul Iman na shule itajengwa Zanzibar, tulimshauri kuwa itakuwa bora badala ya shule kijengwe Chuo Kikuu.

Hivi ndivyo ilivyokuja kujengwa Zanzibar University, Tunguu.

Allah tunakuomba umsamehe dhambi zake mzee wetu huyu na umweke mahali pema peponi.
 
Maalim Mohamed Said ni "KISIMA" cha historia JamiiForums, na ni "TUNU" kwa JamiiForums. Sijawahi kuona member anaemkaribia hata kwa mbali.

Kwa mwenye hekima ni ishara tosha huyu bwana "AMEONA NA KUKUTANA NA MENGI SANA" katika njia ya maisha yake.
 
Maalim Mohamed Said ni "KISIMA" cha historia JamiiForums, na ni "TUNU" kwa JamiiForums. Sijawahi kuona member anaemkaribia hata kwa mbali.

Kwa mwenye hekima ni ishara tosha huyu bwana "AMEONA NA KUKUTANA NA MENGI SANA" katika njia ya maisha yake.
Alexander...
Mji wa Alexandria, Misri umepata jina lake kutokana na Alexander The Great.
Nilifika Alexandria mwaka wa 1988.

Sijapata kuona mji mzuri kupita Alexandria na nimefika miji mingi duniani kama Geneva, Paris, London, New York, Dubai, Johannesburg kwa kutaaja miji michache.

Ahsante sana kaka kwa comments zako.
Hakika nimeona mengi katika maisha yangu.

Tumshukuru Mola wetu.

Hapo chini nikiwa Arab Maritime Transport Academy, Alexandria Egypt.

1606153095613.png
 
Alexander...
Mji wa Alexandria, Misri umepata jina lake kutokana na Alexander The Great.
Nilifika Alexandria mwaka wa 1988.

Sijapata kuona mji mzuri kupita Alexandria na nimefika miji mingi duniani kama Geneva, Paris, London, New York, Dubai, Johannesburg kwa kutaaja miji michache.

Ahsante sana kaka kwa comments zako.
Hakika nimeona mengi katika maisha yangu.

Tumshukuru Mola wetu.

Hapo chini nikiwa Arab Maritime Transport Academy, Alexandria Egypt.

View attachment 1633298
Masha Allah, Allah akujaalie vizazi vyako vipite njia uliopitia maishani (Njia nzuri na njema) na warithi uwezo wa kusoma na kumbukumbu ya wasomayo In Sha Allah.

Hua nikisoma makala zako najiuliza swala moja. Na nimejaribu kukudadavua kwa hilo swala. Kwa karne hii tuliopo, hasa nchini kwetu tanzania;

Wasomi au wajuzi wengi hasa wa "maswala ya kihistoria ya nchi/africa na ya watu mashuhuri nchini/africa", asilimia 99% huzama katika siasa (huishia kuwa wanasiasa) tena mstari wa mbele kwaajili ya maslahi ya kidunia. Ila kwa uwezo ulionao wa sekta ya historia (Ya taifa na watu mashuhuri) nimeshangaa na bado nashangaa hujazama katika hilo kundi!!!

Au pengine nimekosa majibu kwasababu sijui "BACKGROUND" yako kwa undani.
 
Masha Allah, Allah akujaalie vizazi vyako vipite njia uliopitia maishani (Njia nzuri na njema) na warithi uwezo wa kusoma na kumbukumbu ya wasomayo In Sha Allah.

Hua nikisoma makala zako najiuliza swala moja. Na nimejaribu kukudadavua kwa hilo swala. Kwa karne hii tuliopo, hasa nchini kwetu tanzania;

Wasomi au wajuzi wengi hasa wa "maswala ya kihistoria ya nchi/africa na ya watu mashuhuri nchini/africa", asilimia 99% huzama katika siasa (huishia kuwa wanasiasa) tena mstari wa mbele kwaajili ya maslahi ya kidunia. Ila kwa uwezo ulionao wa sekta ya historia (Ya taifa na watu mashuhuri) nimeshangaa na bado nashangaa hujazama katika hilo kundi!!!

Au pengine nimekosa majibu kwasababu sijui "BACKGROUND" yako kwa undani.
Alexander...
Amin.
 
Back
Top Bottom