Alitaka kuuawa kwa sababu yeye ni Mzalendo kwa Chedema?

kunowa

Member
Joined
Oct 30, 2024
Posts
33
Reaction score
46
Wafuasi wa Lissu wanashikilia kuwa Lissu anastahili kupewa uenyekiti wa CHADEMA kwa sababu moja wapo ni kuwa mzalendo wa chama aliyepoteza damu yake kwa ajili ya CHADEMA.

Swali langu: Je, Lissu alipigwa risasi kwa sababu ya kuipigania CHADEMA? Alikuwa anaipigania CHADEMA kwa lipi hasa?

Je, tangu CHADEMA ianzishwe haijawahi kuwa na mpambanaji mwingine zaidi ya Lissu? Ikiwa wapo waliopigania chama kwa dhati, kwa nini wao hawakuwahi kupatwa na tukio kama hilo?

Kwa maoni yangu, Lissu alikuwa anawindwa si kwa sababu ya mapambano ya CHADEMA, bali kwa sababu ya misimamo na matendo yake binafsi. Alionekana kama mtu aliyesaliti taifa kwa kusimama upande wa adui. Hata kama taifa lilifanya makosa kuhusu suala la Makanikia, Lissu alipaswa kutoa ushauri kwa njia bora zaidi badala ya kutumia kila fursa kujijenga kisiasa.

Tatizo lake kubwa lilikuwa tabia ya kuchukulia kila jambo kama nafasi ya kujitengenezea umaarufu wa kisiasa. Kila mara alihutubia hadharani kwa lengo la kupata makofi na kushangiliwa, hata katika mambo yasiyohitaji siasa.

Katika hali hiyo, Lissu hawezi kuchukuliwa kama mzalendo wa taifa, na hivyo pia haiwezi kudhaniwa kuwa mzalendo wa CHADEMA. Badala yake, yeye ni mwanasiasa anayedhani anaweza kushika dola kwa msaada wa mataifa ya nje. Lakini, kama tunavyojua, hakuna msaada wa bure kutoka nje – kuna gharama kubwa inayokuja baadaye. Mataifa ya nje huweka masilahi yao mbele ya yote.

Mfano wa nchi kama Libya na matatizo ya diaspora ni ushahidi wa jinsi uingiliaji wa nje ulivyoharibu baadhi ya mataifa. Lissu anapaswa kujifunza kutoka kwa wanasiasa kama mpinzani wa Museveni nchini Uganda, ambaye hajawahi kuikimbia nchi yake au kutegemea mataifa ya nje. Hata Raila Odinga wa Kenya hajawahi kuacha Wakenya wakimheshimu.

Mwanasiasa kama Lissu si wa kuleta mageuzi ya kweli nchini Tanzania. Badala yake, yupo kwa ajili ya kuvuruga utulivu na amani ya nchi. Taifa halitapata nafuu ya maisha ikiwa kila siku ni chuki, vurugu, na migawanyiko. Amani na mshikamano wa kitaifa ni msingi wa maendeleo na maisha bora kwa wote.
 
Simpendi lissu ktk kupewa chair main lkn hii siikubali
 
Damu yenyewe imejaa mafuta ya alizeti
 
Kupigiwa risasi siyo kigezo Cha uongozi
 
Hata akibaki Mbowe na Odero Odero atashinda Mbowe 20+yrs amechokwa.
 
Swali la kipuuzi sana ,tena san mkuu
 
Swali la kijinga. Uliza swali lingine
 
Hakuna asiyetumia damu au nguvu kati ya mbowe na lissu kukisaidia chadema, wote wametumia, ila kwa sasa lissu ndo anastahili kuliko mbowe, mbowe kapiga 20+ years, lakini lissu kapiga 0 years kama mwenyekiti .Lissu apewe nafasi kwanza tuone mchango wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…