Mh...msemo huu ulikuwa fundisho kwa wale waliopata madaraka ulani na wanayatumia vibaya/kuumiza wenzao.
Hivyo, ni kumbusho tu kwa wale wanaoonewa (waliochini) kwa usihangaike kumloga, kumkaidi, kupoteza muda wako kujaribu kumshusha..,mwisho wa siku atarudi chini tu kwani wazungu wanasema, "Corruption may take you to the top, but it takes character to keep you there"
Haimanishi, ukae chini unamgoja ashuke halafu basi. Kwani pia walisema, "mvumilivu hula mbivu" na "mchumia juani hulia kivulini" endelea kuchumia huko juani kwani ama kwa hakika wakati atakaposhuka, Mungu atakupandisha kwa halali...