Aliyeandika wimbo wa “kajiandae” wa Ommy Dimpoz na Ali kiba ajitokeza! Adai hajalipwa pesa!

Aliyeandika wimbo wa “kajiandae” wa Ommy Dimpoz na Ali kiba ajitokeza! Adai hajalipwa pesa!

mr gentleman

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2012
Posts
3,222
Reaction score
4,689
Zimetufikia za kunyapia nyapia kutoka shirika la wambea SHILAWADU kuihusu hitsong ya wakali wawili wa muziki hapa Bongo Ommy Dimpoz na Alikiba na ngoma yao ya Kajiandae.

Inasemekana kuna mtu afahamikae kama Devi Zinda ambaye anadai kuwa kauandika wimbo huo na hapo awali alilipwa shilingi za kitanzania Laki 5 (500,000) na Ommy Dimpoz kama malipo ya wimbo huo na kuahidiwa kumaliziwa kitita kingine cha shilingi laki 5 ili kutimia million 1 kama ilivyokuwa makubaliano ya malipo ya uandishi wa wimbo huo.

Devi Zinda amepiga story na Soudy Brown leo hii kwenye U-Heard ya XXL na kutoa malalamiko yake yote juu ya Ommy Dimpoz kwasababu anadai kuwa amemtafuta bila mafanikio.
Ubuyu kamili kuhusiana na issue hiyo nimekuwekea hapa chini kwenye video hii, play ili kumsikiliza Devi Zinda akifunguka kwa uchungu kuhusiana na issue hiyo.

 
Na bora tu wasimlipe, wimbo gani huo !!!!!!!! m'baya.
 
Ndo maana ile verse ya Kiba mbaya sana kumbe kaandikiwa [emoji3]
 
yani kuandka tu nymbo ya dkk3 kala la tano na anadai 5nyngne, mbona huku kitaa nawaandkia numbo kwa efu30
 
kwa huo wimbo nawapongeza kwa kutomlipa.
 
Kwa mashairi gani udai mil 1? Ningekuwa mi ndo Ommy Dimpoz ningemdai hiyo laki 5 niliyompa nimuachie elfu 50, kwanza kanyimbo kenyewe kabaya huoni haya kuomba hela?
 
Kwa hiyo sasa sisi tufanyeje? au unataka tumchangie hiyo iliyobaki?
 
Tanzania ina wanamuziki watatu tu
Ben pol
Barnaba
"Rama d"

Hawa wengine wajanja wajanja tu.. "Kiki" za kijinga zinawapaisha!
 
Back
Top Bottom