Bawabu wa pili
Senior Member
- Nov 14, 2025
- 147
- 433
📍DODOMA - Yohana Mathias, Mkazi wa Nzuguni B, amefariki dunia asubuhi ya leo baada ya kuugua kwa muda mrefu tatizo la tezi dume lililoambatana na kupooza kwa sehemu kubwa ya mwili wake.
Kifo cha Mathias kinatokea siku chache baada ya Jambo TV kuchapisha habari akiomba msaada wa matibabu, akiwa amelazwa kitandani kwa zaidi ya Miezi 8 kufuatia changamoto hiyo ya kiafya.
Soma pia: Serikali ya Tanzania imempiga Marufuku Dawa ya Kutibu Maradhi ya Uvimbe WaTezi Dume ya Dr Samsung Misango Asiuze.Kwani Anaharibu biashara ya vidonge
Kwa mujibu wa maelezo aliyoyatoa awali, alidai kuwa safari ya ugonjwa wake ilianza baada ya kugundulika kuwa na tatizo la tezi dume na kuanza kupatiwa matibabu hospitalini.
Hata hivyo, hali yake ilibadilika ghafla baada ya kuchomwa sindano ya matibabu ambayo hakufahamishwa ilikuwa ya nini, hali iliyosababisha kupooza kwa mwili wake na kumfanya ashindwe kuendelea na shughuli zake za kila siku.
Kutokana na ukosefu wa uwezo wa kifedha, Mathias alishindwa kuendelea na matibabu ya rufaa na kulazimika kurejea nyumbani, ambako aliendelea kuishi na maumivu makali hadi umauti ulipomkuta.
Jana Januari 25, 2026 Jambo TV ilipokea maelekezo kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Mtumba na Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, yakielekeza timu kufika leo kwa ajili ya kutafuta usafiri wa kumchukua Mathias na kumpeleka Hospitali ya Benjamin Mkapa kwa matibabu zaidi. Hata hivyo, wakati jitihada za kutafuta gari zikiendelea asubuhi ya leo, taarifa za kifo chake zilipokelewa kabla ya msaada huo kutekelezwa.
Akizungumza kwa niaba ya familia, Mke wa marehemu, Bi. Khadija Ramadhani, ametoa shukrani kwa watu wote waliotoa michango, dua na faraja katika kipindi chote cha Ugonjwa wa mume wake, akisema msaada huo uliwapa nguvu kubwa katika wakati mgumu walioupitia.