Aliyedai anaweza kuunga mfupa uliovunjika bila upasuaji amsaidie Gerald Mdamu

Hii kitu nasikia ipo. Mimi ndugu yangu amevunjika juzi na ameenda kuungwa mfupa Njombe na nasikia mtaalamu mwingine yupo Iringa. Ameambiwa baada ya siku kumi atapona kabisa. Baada ya siku 10 zijazo nitakuja kutoa mrejesho wa hii tiba.
 
Hizo tiba ni kiboko kweli kweli, Boda boda wengi nidipo wanapo tibiwa pindi wapatapo ajali!
 
Huyu mkuu hata mimi namfahamu ni mtaalamu haswa wa mambo hayo yupo kk kwa mbele ukiwa unaenda chuo magereza mpaka kijiji kimoja kinaitwa ikuti nadhani anaitwa malebheja kama sijakosea
 
Huyu mkuu hata mimi namfahamu ni mtaalamu haswa wa mambo hayo yupo kk kwa mbele ukiwa unaenda chuo magereza mpaka kijiji kimoja kinaitwa ikuti nadhani anaitwa malebheja kama sijakosea
Yuko mbele ya ikuti panaitwa Luswisi, luswisi ni ramani ila anaweza akawa anatokea vitongoji jirani na luswisi
 
WaTz tunapenda sana USHIRIKI NA.... Mmekunywa KIKOMBE CHA BABU WA LORIONDO afu mnakuja kukataaa CHANJO ya Mama!
 
Uko sahihi mkuu mimi ni mwenyeji wa tukuyu
 
Mpigieni mwenye namba hii
0713285617
Alinitibu mimi baada ya kuteseka sana.
Anachotaka ni kumpeleka X-Ray ya mgonjwa ili aangalie mfupa umevunjikaje.
Ana Kibali cha Wizara ya afya, analaza hadi wagonjwa.

Mimi niliteseka miaka miwili huku pesa nikiwa nayo.
Alinitibu kwa mwezi mmoja tu nikapona kabisa.

Mpigieni atamsaidia mgonjwa.
 
Wapo wengi sana hasa mkoa wa Mara sasa nani atahakikisha Gerald amefikishwa hapo ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…