GE2025 Aliyedhalilisha Jeshi kwa kuliweka mitaani kabla ya Uchaguzi afunguliwe mashtaka ya "kudhalilisha Jeshi" na "Uhaini"

GE2025 Aliyedhalilisha Jeshi kwa kuliweka mitaani kabla ya Uchaguzi afunguliwe mashtaka ya "kudhalilisha Jeshi" na "Uhaini"

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

The Father of All

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Posts
11,099
Reaction score
13,709
Kazi ya JWTZ ni kulinda mipaka ya Tanzania na watanzania dhidi ya maadui wa nje.

Mosi, ni bwege na zwazwa gani ameamuru jeshi liingie mitaani kuingilia kazi ya polisi?

Pili, walishuku kuwa polisi hawana morali, hivyo, wasingetimiza wajibu wao?
Tatu, kuna uoza na uzwazwa zaidi ya huu?

Nne, licha ya amiri jeshi wake, nani anaweza kuliamuru jeshi kuingia mitaani na kuingilia kazi ambayo si yake kikatiba?

Tano, jeshi nalo litakubali kudhalilishwa na kutumiwa vibaya dhidi ya wananchi linalopaswa kuwalinda na kuwasikiliza?

Sita, nani atapewa adhabu ya uhaini huu ili kutoa somo uzwazwa na uhaini huu uisirudiwe?
Saba, mhusika alizingatia maslahi au maumivu ya nani?
Nane, kama hajui dhima na uzito wa dhamana yake, anafaa kuendelea kuwa amiri jeshi kweli?
Tisa, nini madhara ya uzembe huu kwa taifa?
Kumi, nani atapewa adhabu ya uhaini huu ili kutoa somo uzwazwa na uhaini huu uisirudiwe?
 
Kazi ya JWTZ ni kulinda mipaka ya Tanzania na watanzania dhidi ya maadui wa nje. Ni bwege na zwazwa gani ameamuru jeshi liingie mitaani kuingilia kazi ya polisi? Je, walishuku kuwa polisi hawana morali, hivyo, wasingetimiza wajibu wao? Je, kuna uoza na uzwazwa zaidi ya huu? Je, licha ya amiri jeshi wake, nani anaweza kuliamuru jeshi kuingia mitaani na kuingilia kazi ambayo si yake kikatiba? Je, jeshi nalo litakubali kudhalilishwa na kutumiwa vibaya dhidi ya wananchi linalopaswa kuwalinda na kuwasikiliza? Je, nani atapewa adhabu ya uhaini huu ili kutoa somo uzwazwa na uhaini huu uisirudiwe?
So far, JWTZ hawajaingia huo mtego wa kutumiwa na wanasiasa wahuni. Hawajatoa amri yoyote ya kutawanya waandamanaji. In fact, uwepo wao kwa kiasi fulani umeleta hamasa kwa protesters! JWTZ ndiyo chombo pekee kinachoaminiwa na umma wa Watanzania.
 
Mimi mama Samia ndio nimewaagiza wanajeshi waingie mtaani
 
JESHI KUTUMIWA NA SERIKALI ?

Mtego mbaya wa serikali kujaribu kutumia jeshi la ulinzi wa taifa kisha likawageuka watawala wa chama dola kongwe kilichotaka kubaki madarakani kwa ubabe

TOKA MAKTABA :

Katika mahojiano exclusive Luteni Mwamba Luchembe anafunguka miaka mingi baadaye nini kilimsukuma kuvamia studio za Shirika la Habari la Zambia ZBC mwaka 1990 kutangaza mapinduzi ya kungoa serikali ya chama dola UNIP iliyokuwa inaongozwa na Rais Kenneth Kaunda baba wa taifa hilo.

27 May 2022
Luteni Mwamba Luchembe, Tuliitwa kusaidia polisi walioshindwa kuzima maandamano

View: https://m.youtube.com/watch?v=yY6JDPWaHuY
Former Zambian army officer Mwamba Luchembe reflects on the day he tried to overthrow Kenneth Kaunda in a military coup. (This interview was recorded while PF were in power and Kenneth Kaunda was still alive.)
Tulikuwa katika kambi yetu kilometa 500 kutoka mji mkuu wa taifa la Zambia, jiji la Lusaka.

1990 hali ya kisiasa na kiuchumi ilikuwa mbaya, wananchi walikuwa na manunguniko mengi ikiwemo ugumu wa maisha, ughali wa bidhaa muhimu kama unga wa sembe, ukandamizaji wa kisiasa uliokuwa unafanywa na chama dola kongwe kimoja UNIP

Maandamano yakatokea jeshi la Polisi likatumwa kudhibiti mandamano hayo lakini wakazidiwa na nguvu ya umma uliojitokeza .

Rais Kaunda akatoa amri jeshi la ulinzi la Zambia watoke kambini kuongeza nguvu kudhibiti maandamano.

Hivyo mimi nilikuwa katika Battalion 5 Kaoma, nasi tukapewa amri tuende Lusaka kuongeza nguvu kudhibiti maandamano.

Wakati tukiwa mesi tunakula chakula cha jeshi ambacho hatulipii, mawazo yetu yakaguswa na madhila ya wananchi wasiokuwa na uwezo wa kula ambao walijitokeza kwa wingi kuandamana huku sisi tukila chakula kwa uhakika kupitia kodi zao.

Hivyo tukaona nchi inaenda kubaya kutokana na kuwa na chama kimoja kongwe tawala kilichoishiwa mawazo ya kutanzua changamoto za raia.

Wazo letu likawa kuchukua nchi na kuiongoza kwa miezi sita huku tukijenga mazingira vyama angalau vitatu makini viundwe ili demokrasia iwepo nchini. Hatukutaka kuona vyama zaidi ya vitatu maana tunajua vyama vingine ni vya mfukoni ( briefcase) siyo vyama vya ukweli vya mawazo mbadala

Tukiamini demokrasia ya uwazi, uchaguzi huru, bunge makini vingeweza kuiondoa nchi ktk changamoto iliyokuwa nchi inapitia ...

Ndiyo maana niliongoza platoon iliyokuwa na wanajeshi 32 huku mimi ni kiwa ofisa wao hivyo jumla ya wanajeshi 33 tulivamia kituo cha taifa cha ZBC nami nikatoa tangazo la serikali kupinduliwa...

Tulikuwa tumekubaliana na kambi zingine za Kitwe, Mufulira n.k nao waingie ktk sehemu nyeti za utawala wa kiserikali ktk majimbo ili kukamilisha mapinduzi hayo...

Wananchi walijitokeza kwa wingi mtaani kufurahia tangazo la mapinduzi ya kijeshi. Hata hivyo wenzetu tuliokubaliana kuikamilisha kazi hivyo kote nchini walitugeuka.

Akatumwa askari mmoja mwandamizi atushawishi kuwa mapinduzi yetu hayakufanikiwa.

Nilikamatwa na kupelekwa kituo kikuu cha Central police nikafungiwa katika mahabusu upande wa wanawake, na wale mahabusu wote wanawake kwanza walihamishwa.

Wakaja wanajeshi wa idara ya utambuzi, maofisa wa usalama wa taifa na wa vyombo vingine kunihoji kwa muda wa wiki moja ktk selo hiyo ya wanawake.

Baada ya hapo walinipakiza ktk helicopter tukaelekea katika kambi nilitotokea iliyopo kilometa 500 kutoka Lusaka. Wakafanya upekuzi katika ofisi nikiyokuwa natumia kambini na katika nyumba niliyokuwa naishi kambini.

Wakanirejesha Lusaka hata hivyo usiku ulikuwa umeanza kuingia hivyo rubani wa helicopter akazima mawasiliano yote na kutua eneo mojawapo kwani rubani alitoa taarifa ya kuwa helicopter haina uwezo wa kusafiri usiku wa giza kufika Lusaka. Walizima mawasiliano ili kama kuna njama za wenzangu kuja kuniokoa zisifanikiwe.

Alfajiri na mapema tukamalizia safari yetu kwa usafiri wa barabara hii yote ikiwa ni njia ya medani, kwa waliopanga nami kufanya mapinduzi wasijue nilipo wala nini kimetokea kwangu mimi.

Mahojiano yakaendelea mjini Lusaka ktk nyumba maalum (safe house) kujaribu kupata habari zote za Mapinduzi na wahusika wote katika njama hii ya kupindua nchi.

Walitumia koleo / pliers kutoa meno yangu kavukavu bila ganzi, lakini situwasaliti wala kutaja wenzangu waliotayarisha jaribio la kuangusha serikali.

Baada ya kunisulubu hivyo, wakanirudisha kwa kificho kituo kikuu cha Polisi huku nikiwa na maumivu makali. Wakanipandisha ghorofani, watu wa Idara ya Usalama na wale wa Idara ya Utambuzi jeshini wakapanga mipango watawaambia nini raia hata polisi na wanajeshi watakaoniona.

Hivyo basi wakanivua nguo zote tukiwa ghorofani na kuzitupa kupitia dirishani. Kutoka juu ghorofani wakanitelemsha mzobemzobe mbiombio uchi wa mnyama nikiwa mtupu, kisha wale wote walikuwapo kituo kikuu cha Polisi wakanishangaa si polisi, raia na waandishi wa habari hata wapita njia wakabaki wanajiuliza kulikoni..

Watu wa Idara na Vyombo wakasema huyu ni kichaa aliyewehuka siku nyingi kabla ya mapinduzi, faili lipo jeshini na kwa vile alikunya sana Pombe na bangi ndiyo maana akatimka kwenda, kutangaza mapinduzi yale.

Baada ya miezi miwili nikastaafishwa jeshi kwa sababu za 'kiafya' yaani ugonjwa wa akili. Hata hivyo vyombo vya usalama vikamwambia rais pamoja na hii hadaa tuliyoitengeneza ukweli watu wanataka na wanaamini mabadiliko ya kuleta vyama vingi vya kisiasa. Hivyo ni bora rais aanzishe mchakato wa mabadiliko ya katiiba kuruhusu na kuafiki kwa moyo mkunjufu vyama vingi, demokrasia na uchaguzi huru kupitia tume huru ya uchaguzi.

Hivyo mwaka 1991 mchakato wa vyama vingi na katiba mpya vikapitishwa na bunge la Zambia kwa usimamizi wa karibu wa rais Kenneth Kaunda.

Mapinduzi yale yaliyoshindwa hata hivyo yalileta jambo chanya kuwa watu wanataka mfumo wa vyama vingi, yalionesha kuwa ukiritimba wa chama dola kongwe cha UNIP na rais nguvu yao ya ushawishi wa chama kimoja umepungua na wajitayarishe kuwa chama cha upinzani.

Kwa ujasiri wa Luteni Mwamba Luchembe kuongoza jaribio la mapinduzi , sasa anahesabika kama baba wa mabadiliko / reforms za kupatikana katiba mpya na demokrasia ya vyama vingi nchini Zambia.

Katika mitaala vya masomo ya uraia / civic Luteni Mwamba Luchembe anatokea ktk vitabu mashuleni kuwa alikuwa chachu ya mabadiliko yaliyoleta vyama vingi kuruhusiwa nchini Zambia.

Mbali ya watoto wa shule kusomeshwa mchango wake Luteni Mwamba Luchembe kuleta mabadiliko, sasa katika Makumbusho ya Taifa mjini Lusaka na makumbusho ya majimbo mbalimbali nchini Zambia picha yake ipo miongoni mwa watu waliotoa mchango kwa taifa la Zambia hadi kufikia lililopo sasa.

Rais Frederick Chiluba aliposhinda uchaguzi wa vyama vingi kupitia chama cha upinzani alimrejesha Luteni Mwamba Luchembe kazini na kumpa cheo mserereko hadi kuwa Captain kisha kumstaafisha kwa kumpatia pensheni stahiki ya cheo alichofikia.

Source :
 
So far, JWTZ hawajaingia huo mtego wa kutumiwa na wanasiasa wahuni. Hawajatoa amri yoyote ya kutawanya waandamanaji. In fact, uwepo wao kwa kiasi fulani umeleta hamasa kwa protesters! JWTZ ndiyo chombo pekee kinachoaminiwa na umma wa Watanzania.
Hivi si kuna fala mmoja hivi mkuu wa mkoa ambaye aliwahi kuwaamrisha JWTZ kufanya usafi wa jiji, au nimekosea?
 
Kuna la Kujifunza hapa na Ku note, Imenishangaza sana kuona Presence ya wanajeshi asubuhi ili kabisa kwenye maeneo ya maandamano ile Hali ulinzi ulipaswa ufanywe na Polisi!!!

Pili inawezekana pia Jeshi limenusa halafu Fulani ya maadaui wa nje kutumika kwenye maandamano na kuvuruga Amani ndio mana likaja front kulinda Actual protestors ambao ni Watanzania

Bado Kuna Contradiction nyingi sana pamoja na kuwa Sina information zozote Lakini Kuna pattern zina goma Ku connect

I smell something fishy kabisa
 
Polisi wa Tanzania akili zao ni kuua tu sio kulinda watu! DJ walete JW
 
Kuna la Kujifunza hapa na Ku note, Imenishangaza sana kuona Presence ya wanajeshi asubuhi ili kabisa kwenye maeneo ya maandamano ile Hali ulinzi ulipaswa ufanywe na Polisi!!!

Pili inawezekana pia Jeshi limenusa halafu Fulani ya maadaui wa nje kutumika kwenye maandamano na kuvuruga Amani ndio mana likaja front kulinda Actual protestors ambao ni Watanzania

Bado Kuna Contradiction nyingi sana pamoja na kuwa Sina information zozote Lakini Kuna pattern zina goma Ku connect

I smell something fishy kabisa
Mbona kipindi jeshi likipiga jeramba na police,migambo pamoja na magereza hamkuhoji?
 
Back
Top Bottom