Aliyedhaniwa amekufa azinduka akiwa muchwari

Aliyedhaniwa amekufa azinduka akiwa muchwari

kaangwa

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2011
Posts
644
Reaction score
193
Wananchi wa Kenya wameshangazwa na taarifa ya mwanamumemmoja aliyezinduka akiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitalimoja mjini Naivasha umbali wa kilomita tisini kutoka mji mkuu Nairobi.
Mwanamume huyo Paul Mburu mwenye umri wamiaka 24, alipelekwa hospitalini kwa matibabu baada ya kunywa sumu kwa lengo lakujitoa uhai,kutokana na ugomvi wa kinyumbani na babake ingawa alisemekanakufariki Jumatano usiku wakati akipokea matibabu.
Taarifa zinazohusiana

Wafanyakazi wa hospitali hiyo walipigwa nabutwaa na hata kutoroka walipoona mwili wa mtu waliyedhani ni maiti ukisonga nakuonyesha dalili za kuwa hai katika chumba cha kuhifadhia maiti.
Afisaa mkuu wa matibabu katika hospitalihiyo ya wilaya, Dokta Joseph Mburu, alisema kuwa dawa iliyotumiwa kumtibu Mburuhufanya moyo kupiga polepole hali ambayo huenda ilimfanya muuguzi kudhani kuwamgonjwa alikua amefariki.
Mwanamume huyo alisikika akimtaka mmoja wawafanyakazi katika chumba cha kuhifadhia maiti kumsaidia kwani alikuwa anahisibaridi kali na hapo ndipo mmoja wa wafanyakazi alipotimua mbio kwa hofu.
Nusura Mburu awekwe kwenye jokovu lakuhifadhia maiti.
Jamaa za mwanamume huyo akiwemo babakewalikuwa wametembelea chumba cha maiti siku ya Alhamisi ili kujiandaa kwamazishi , lakini baadaye mchana walifahamishwa kuwa Mburu alikuwa hai.
Source: BBC news
Mytake: kwa madaktari je ni sababu zipi zinaweza kusababisha hili au ni miujiza ?

 
Imeandikwa Bwana atafanya jambo jipya!! Jambo ambalo ukisikia masikio yatawasha, ukiona macho yatatoa machozi, na ukiwaza akili haitakubali... Hii ni saa ya ufufuo na uzima duniani.
 
Imeandikwa Bwana atafanya jambo jipya!! Jambo ambalo ukisikia masikio yatawasha, ukiona macho yatatoa machozi, na ukiwaza akili haitakubali... Hii ni saa ya ufufuo na uzima duniani.

Amina, utukufu ni wa Bwana.
 
ni uzembe wa watumishi wa hospital hiyo tu hakuna miujiza hapo
 
Huwa inashauriwa kutokimbizia mochwari mtu anayedhaniwa kufa kwa masaa kadhaa ili asijepelekwa mtu ambaye bado yuko hai.
 
Ingekua ni Zenji sa4 asubuh watu wangekua wanatoka makaburini anabahati sana kwa hiyo kaghairi kujiua au mpango wake upo pale pale?
 
Back
Top Bottom