Aliyefanikisha usajili wa Samatta atupiwa virago nje

Aliyefanikisha usajili wa Samatta atupiwa virago nje

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Klabu ya Aston Villa imemfuta kazi mkurugenzi wake wa michezo , Jesus Garcia Pitarch baada ya kukosoa sera za usajili za klabu hiyo.

Mshambuliaji wa klabu ya AstoNVilla, Mbwana Samatta akimzunguka mlinzi wa Leicester City, John Evance katika mechi ya EPL.

Pitarch aliondoka klabuni hapo siku ya jumatatu ikiwa ni siku moja baada ya timu hiyo kufanikiwa kusalia katika ligi kuu ya England baada ya kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya West Ham United.

Ilifahamika kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo Dean Smith alihakikishishiwa kibarua chake na kuahidiwa kiasi cha fedha kwa ajili ya usajili ingawa klabu ilishaanza kufanya tathmini ya msimu uliomalizika na mikakati ya msimu ujao.

Smith ndiye aliyependekeza usajili wa Tyrong Mings na Tom Heaton ambao walikua na matokeo chanya katika klabu hiyo.

Katika majira ya kiangazi, Villa ilitumia kiasi cha pauni milioni 140 katika usajili huku Pitarch akiwa ndiye aliyehusika katika kuleta wachezaji wakiwemo Wesley Moraes aliyenunuliwa kwa ada ya rekodi ambayo ni pauni milioni 21,Matt Targett,Douglas Luiz ,Marvelous Nakamba na Mbwana Samatta.

Pitarch pia alihusika katika usajili wa Trezeguet raia wa Misri ambaye alifunga mabao matatu katika mechi chache za mwisho zilizoinusuru Villa kuporomoka daraja.

Si taarifa nzuri kwa nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta ambaye tangu asajiliwe kwa ada ya pauni milioni 8 kutoka KRC Genk katika dirisha la usajili la mwezi Januari mwaka huu, amecheza mechi 16 za mashindano yote na kufunga mabao 2 tu.
 
Msimu ujao Samatta ana kazi kubwa sana kupata namba akizembea atapelekwa kwa mkopo au atapigwa benchi.
 
Msimu ujao Samatta ana kazi kubwa sana kupata namba akizembea atapelekwa kwa mkopo au atapigwa benchi.
Samatta huyooo...
Screenshot_20200724-015311_Chrome.jpg
Screenshot_20200724-015332_Chrome.jpg
 
Kwa maoni yangu Villa walisajili wachezaji wazuri sana chini yake. Tatizo ni falsafa yao ya kujenga timu kumzunguka mchezaji mmoja (bwana Grealish). Epl haitaki huo upuuzi. Ndiyo sababu kazi ya wapinzani huwa ni moja tu, kumdhibiti Grealish. Mwaka huu wameponea chupu chupu ila msimu ujao wasipochange moto utawawakia.
 
Ni kweli kabisa J Grealish ndiyo muanzilishi wa mashambilizi mengi. Wakiingia final third mpira anapewa Grealish, akikabwa vizuri, timu imeshindwa.
 
Ligi sio shida. Shida hao Aston villa hawaeleweki. Hazard alikua moto EPL kaenda La liga anaonekana wakawaida.
 
Msimu ujao Samatta ana kazi kubwa sana kupata namba akizembea atapelekwa kwa mkopo au atapigwa benchi.

Kipaji anacho, lakini amekuwa mvivu wa kuujua mpira wa kiingereza ambao ni nguvu nyingi, kukimbia kwingi na matumizi ya akili nyingi katika kuji-position.

Ana muda wa kurekebisha hayo kama kweli anahitaji kubaki uingereza. Mfano mdogo amuangalie mchezaji Connolly wa Brighton anavyohangaika uwanjani. Mpelekeeni salam hizi.
 
Back
Top Bottom