Jannatul Firdaus
JF-Expert Member
- Aug 4, 2026
- 446
- 1,113
Aliyefariki kwa kuongeza uume, ameripotiwa kuwa alifanya taratibu hizo za kuongeza uume mara 5 kati ya mwaka 2024 na 2026.
Igho "Tiny" Ubiribo, raia wa Nigeria na Influencer aliyeishi jijini London, ambaye alifariki dunia tarehe 6 Machi nchini Thailand chini ya saa 24 baada ya kufanyiwa utaratibu wa mwisho wa kuongeza maumbile ya kiume kwa kutumia sindano za hyaluronic acid.
Uchunguzi wa kidaktari ulionyesha kifo chake kilisababishwa na sindano hizo na tatizo la damu kuganda kwenye mapafu (pulmonary embolism).
Kufuatia tukio hilo, Wizara ya Afya ya Thailand ilianzisha uchunguzi mkubwa tarehe 7 Septemba dhidi ya kliniki hiyo ya urembo iliyopo Bangkok ili kubaini kama ilikiuka viwango vya matibabu.
Uongozi wa kliniki hiyo unadai kuwa daktari alimshauri Ubiribo kugawa dozi hiyo ya mwisho katika vipindi viwili tofauti, lakini yeye alikataa na kusisitiza sindano zote zipigwe kwa mkupuo mmoja. Masaa machache baada ya huduma hiyo, alianza kulalamika maumivu ya kifua kabla ya kuzirai.
Licha ya madaktari kujaribu kumsaidia kwa kumpa huduma ya dharura ya kurejesha mapigo ya moyo (CPR) kwa dakika 101, alitangazwa kufariki dunia. Kliniki inajitetea kuwa mteja alisaini fomu za kuridhia matibabu na hakuwahi kulalamika huko nyuma.