Aliyeghushi nyaraka za kesi ya ndoa afungwa miaka 7

Aliyeghushi nyaraka za kesi ya ndoa afungwa miaka 7

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemhukumu kifungo cha miaka saba jela, Tuwaha Muze (44) baada ya kupatikana na hatia katika makosa mawili ambayo ni kughushi makubaliano ya uongo na kuwasilisha nyaraka za uongo za mwenendo wa kesi ya ndoa.

Pia, mahakama hiyo imemhukumu Samson Tuwaha, kifungo cha Mwaka mmoja jela, asitende kosa lolote la jinai ndani mwaka mmoja, baada ya kupatikana na hatia ya kughushi makubaliano ya uongo.

Hukumu hiyo imetolewa leo Jumatatu, Novemba 14, 2022 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Hakimu Mkazi Mkuu, Romuli Mbuya, wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya hukumu.

Hakimu Mbuya alisema mahakama imewatia hatiani washtakiwa hao baada ya upande wa mashtaka kuwasilisha mashahidi wanne.

Alisema Muze atatumikia kifungo cha miaka mitatu na nusu kwa kila kosa na hivyo adhabu yake itakwenda kwa pamoja ambapo atatumikia kifungo cha miaka saba jela bila faini.

Mahakama imezingatia maombi yake ya ugonjwa na umri mkubwa, Mahakama inakuhukumu kifungo cha nje cha mwaka mmoja kwa kutojihusisha na kosa lolote la jinai katika kipindi hicho.

Awali, kabla ya kutolewa hukumu hiyo Wakili wa Serikali, Tumaini Mafuru aliomba mahakama itoa adhabu kali dhidi ya washtakiwa hao ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia hiyo.

Kabla ya huku, Muze kupitia wakili wao, Alexander Mzikila aliomba wapunguziwe adhabu kwa kuwa ana mke na watoto wanne wanaomtegemea.

Naye Samsoni aliomba mahakama impunguzie adhabu na kwa sababu anasumbuliwa na ugonjwa wa Kisukari, presha na amefiwa na mke wake.

Hakimu Mbuya alisema kwa makosa hayo, mshtakiwa akitiwa hatiani adhabu yake ni kifungo kisichopungua miaka saba jela.

Akipitia ushahidi wa upande wa mashtaka, alisema mlalamikaji katika kesi hiyo Maimuna Soka (aliyekuwa mke wa Muze) alisafiri kikazi na aliporudi alikuta mipango ya nyumba yao ya Ghorofa moja imebadilishwa vitasa kwa kiwekea vitasa vipya na Ikiwa haina mtu na watoto wamepelekwa kwa baba yao Kimara bonyokwa.

Hakimu Mbuya alisema katika ushahidi wake Maimuna, alidai kuwa Julai 2017 alisafiri kikazi kwenda mikoa ya Lindi, Mtwara na Songea.

Maimuna alidai aliporudi Dar es Salaam, alifika Majira ya saa tisa na kuelekea nyumbani kwake Mbezi Luis.

Alidai alipofika nyumbani kwake alikuta nyumba yake imebadilishwa vitasa na watoto wake wawili nao walihamishwa kutoka katika nyumba hiyo kwenda kwa wazazi wa mume wake huku mlizi aliyekuwa analinda nyumba yao, akimkatalia kuingia ndani ya nyumba yake.

Baada ya kuona hivyo alimpigia simu mme wake lakini hakupokea simu, alienda kuripoti kwa mjumbe wa nyumba 10.

Mjumbe huyo wa nyumba kumi aitwaye Hariet Mapunda alimpeka kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mbezi Luis.

"Tulipofika kwa mwenyekiti, mjumbe alimueleza Hali halisi na ndipo Mwenyekiti yule alimpigia simu mume wangu na mume wangu alipokea simu na kuelekeza funguo zilipo, ambapo alisema funguo zipo kwa baba yake mzazi anayeishi Kimara Bonyokwa" alidai Maimuna na kuongeza

"Mwenyekiti alinishauri niende nikazichukue funguo huko Kimara Bonyokwa kwa baba mkwe na hivyo tuliongozana mimi, mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa zamani na mjumbe," alidai

Kwa upande wake, shahidi wa nne wa upande wa mashtaka, Colman Kimaro ambaye ndio aliyewauzia kiwanja alidia Maimuna na mume wake Muze ndio waliofika kwake wakitaka kiwanja cha kununua na alipowauzia hakukuwa na mtu mwingine zaidi yake, hivyo anashangaa kuona Muze anadai ghorofa hiyo Mali ya baba yake.

Katika ushahidi wake Muze, alidia nyumba ya ghorofa aliyokuwa anaishi yeye pamoja na mke wake, kabla ya kutengana ilikuwa mali ya baba yake mzazi, aitwaye Samson Tuwaha Muze.

Muze alidai kuwa Januari 2010 alifunga ndoa ya bomani na mke wake aitwaye Maimuna Soka, ambaye alikuwa anafanya kazi Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Kibaha Mizani.

Alidai baada ya muda mfupi mke wake alipata kazi ya muda, hivyo alipomwomba nyumba ya kukaa baba yake mzazi ambaye ni mshtakiwa wa pili katika kesi hii (Samson Tuwaha)

Aliendelea kudai kuwa baba yake alikuwa anafanya kazi mkoani Tanga na alikuwa na nyumba nyingi, hivyo aliomba wapewe moja kwa ajili ya kukaa na mke wake, Jambo ambalo baba yake huyo aliridhia na kumtaka wakae kwa muda.

"Baba alitupa nyumba ya Kimara Bonyoka, lakini sisi tulimuomba atupatie nyingine kwani huko barabara ilikuwa mbaya na kutokana na hali ya mke wangu kuwa mjamzito, isingetufaa ndipo alipotupa nyumba ya ghorofa moja iliyopo Mbezi Luis na aliomba makabidhiano yafanyike kwa mwanasheria nababa mdogo ambaye kwa sasa alishafariki dunia," alidai

Alidai baba yake alimueleza kuwa wakae katika nyumba hiyo kwa muda kwa sababu yeye anakaribia kustaafu hiyo atahitaji kuja kuishi katika ghorofa hiyo.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, Muze na baba yake wanadaiwa kughushi makubaliano ya uongo ya upangaji wa nyumba ya ghorofa moja iliyopo Mbezi Luis, wakionyesha kuwa nyumba hiyo ni mali ya Samson, wakati wakijua kuwa ni uongo na nyumba hiyo ni mali ya Maimuna Soka na aliyekuwa mume wake, Tuwaha Muze.

Shtaka la pili, linamkabili Muze pekee yake, ambapo anadaiwa kuwasilisha mahakamani nyaraka za uongo za mwenendo wa kesi ya ndoa namba 66/ 2017, katika mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, wakati wakijua nyaraka hizo ni za uongo.

MWANANCHI
 
Kuna mdau alianzisha thread hapa akasema ndoa ni kaburi linalotembea.
 
Mali ni upuuzi tu. Huyu akitoka atakuwa anajuta. Miaka 7 alipaswa kutumia kuhangaikia ghorofa jingine
 
nchi hii inawatu wa hovyo Sana unawezaje kuidanganya mahakama kirahisi hivyo ukijua wazi ili nyaraka ya nyumba ikamilike ni mchakato
 
Back
Top Bottom