Aliyegongwa na mwendokasi atambuliwa na mkewe na ndugu yake

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731

Mtembea kwa miguu aliyegongwa na Basi la Abiria la "Mwendokasi" wiki iliyopita ambaye ndiye alikuwa Majeruhi pekee wa ajali hiyo aliyesalia katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI), ametambulika ambapo jina lake ni Osam Milanzi, Mkazi wa Manzese Midizini.

Meneja Uhusiano wa MOI @taasisiyamifupa_moi , Patrick Mvungi amesema utambuzi huo umefanywa na Mke wa Majeruhi huyo(Osam) aitwaye Isha Mohamed pamoja na Mdogo wa Osam anayeitwa Shaban Milanzi. (Kwenye swipe kuna picha ya Mvungi akiwa na Mke wa Osam ambaye amesimama katikati pamoja na Ndugu wengine wa Osam)

Mvungi amenukuliwa akisema “Afya ya Osam imeimarika sana kutokana na kazi kubwa ambayo imefanywa na Madaktari, Wauguzi pamoja na Watumishi wengine wa MOI, MOI tunatoa shukrani za dhati kwa vyombo vya habari pamoja na Watanzania wote wenye mapenzi mema ambao walishirikiana nasi kutangaza habari za kuwatafuta Ndugu wa Osam”

Itakumbukwa jana Hospitali hiyo ilitoa taarifa kwamba Osam tayari ameondolewa katika Chumba cha Uangalizi Maalum (ICU) na kuhamishiwa wodi nyingine ya HDU baada ya afya yake kuzidi kuimarika ambapo pamoja na mambo mengine Majeruhi huyo ameanza kuongea na amejitaja kwa jina moja kwamba anaitwa Osam na Makazi yake ni Manzese, Dar es salaam.

Pia soma:
 
Huyo kijana mmoja pichani kapiga picha utadhani krismass.
 
Yaani kama yuko hai mpaka leo sina cha kusema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…