Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Meneja Uhusiano wa MOI @taasisiyamifupa_moi , Patrick Mvungi amesema utambuzi huo umefanywa na Mke wa Majeruhi huyo(Osam) aitwaye Isha Mohamed pamoja na Mdogo wa Osam anayeitwa Shaban Milanzi. (Kwenye swipe kuna picha ya Mvungi akiwa na Mke wa Osam ambaye amesimama katikati pamoja na Ndugu wengine wa Osam)
Mvungi amenukuliwa akisema “Afya ya Osam imeimarika sana kutokana na kazi kubwa ambayo imefanywa na Madaktari, Wauguzi pamoja na Watumishi wengine wa MOI, MOI tunatoa shukrani za dhati kwa vyombo vya habari pamoja na Watanzania wote wenye mapenzi mema ambao walishirikiana nasi kutangaza habari za kuwatafuta Ndugu wa Osam”
Itakumbukwa jana Hospitali hiyo ilitoa taarifa kwamba Osam tayari ameondolewa katika Chumba cha Uangalizi Maalum (ICU) na kuhamishiwa wodi nyingine ya HDU baada ya afya yake kuzidi kuimarika ambapo pamoja na mambo mengine Majeruhi huyo ameanza kuongea na amejitaja kwa jina moja kwamba anaitwa Osam na Makazi yake ni Manzese, Dar es salaam.
Pia soma: