Aliyeharibu Maths ionekane ngumu

Wana jamvi embu leteni maoni yenu juu ya huku ugumu wa maths nani amechangia kwa kiasi kikubwa..mm hasa naona ni ALGEBRA yeye ndie ameleta uhasama kwenye maths baada ya kuchanganya herufi na namba..

3x+y=10
4y-x=4

Find the sum of x and y
 
Chemistry wao wakalazimisha eti ubalance number na herufi......I was like whaaaaaat!!? Mara balance chuma na hewa Mara h2o+h2 = O2+h+ niliona maruwe tu
 
Hata kukariri ni ujanja wa kushinda shule.
 
Math's na masomo mengine ya sayansi ni mazuri ila tatizo mbinu za kisasa za ufundishaji ndio shida...Waalimu wa sayansi wengi ni waliofeli. Ni aghalabu kukuta Mwalimu alifaulu kwa daraja A ktk somo analofundisha. Mfano mzuri Math's ni kama Game lakini Mwl akianza kufundisha ataanza kwa mikogo na vitisho wakati ukianza kumfundisha mwanafunzi kama game basi ataipenda na atakuwa ni mchezaji mzuri wa game hiyo!

Wito wangu Walimu wa Sayansi tuache mbwembwe za kuwatisha watoto katika masomo haya kwani kama yalikuwa magumu kwetu tusiwakririshe ugumu ule, Tujitahidi kuwarahisishia zaidi kwani watoto wa sasa wanaupeo mkubwaa saana na ni wadadisi saana kwao Math's si MZIGO TENAAAA!!!!!!
 
Hesabu kwangu km kumsukuma mlevi tu .....sikuwa napiga tizi sana..sikuwa naenda sana class lakini natisua tu kwa uwezo binafsi
Nina F ya Civics lkn Maths nna credit....inategemeana na mtu mwenyewe...kwangu hesabu ngumu zilikuwa zile cjui za "predictation" unachorachora vitawi eti kutafuta jibu sijawahi Fanya mabisa
 
Teh teh teh,
unakumbuka H He Li Be B C Na O F Ne ...............................................................
He He. Lile Beda Bovu Chonya Nipe Orange Fanta Nende. Na Muganyizi Alivuta Sigara Packet Sita Arusha.....
Hahahaa, Muha akaongezea: Kiswahili Cha Ghana Geresha, Asha Sema British Kiropa.... Bado nakumbuka na inasaidia.

Beda lilikuwa bakuli la uji, Chonya alikuwa Mpishi pale Mazengo Sec na Muganyizi alikuwa Mwalimu na Dj wetu mkali sana.
 
baada ya kujua hizi halama(+ - x na kugawanya) na matumizi yake sina shida tena na mambo ya logarithm sijui ALGEBRA kuniumiza kichwa tu
 
Huyo algebra kweli fala namba uweke na herefu alafu utuulize hizo herufi ni namba zipi

Ujinga ndio maana mambo ya kijinga yalinishinda
haaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
maths ni kipaji wala hailazimishwi..huwa inakuwa automatic kwa MTU ukijifanya unang'ang'ania no longer una burst kichwa
 
Katika masomo nayoyachukia duniani hesabu number moja
 
Ni mwali Sigi ndo aliharibu kabisa..simpendi kama nn na yale maswali yake ya Geometry,kuna mafumbo humo cjui unajaza page tatu..huku bado kaingia na rundo la fimbo...waai mimi sitaki kabisa Mathematics
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…