Aliyehoji uraia wa Askofu Niwemugizi kuzikwa na Askofu Niwemugizi

Aliyehoji uraia wa Askofu Niwemugizi kuzikwa na Askofu Niwemugizi

BIN BOR

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2010
Posts
1,013
Reaction score
407
Askofu Niwemugizi alipotumia uhuru wake wa kutoa maoni, kufumba na kufumbua, makachero wakamvaa na kumpora pasi ya kusafiria. Wakauliza, "Wapi kaburi la bibi ya babu yako?"

Sasa kabla Baba Askofu hajaanza ibada ya mazishi, mrudishieni kwanza pasi yake ya kusafiria.

Soma hapa:

1) Askofu Niwemugizi wa Kanisa Katoliki aitwa Uhamiaji kuhojiwa juu ya uraia wake

2) Uraia wa Askofu Severine Niwemugizi (mkosoaji wa Serikali) unaendelea kuchunguzwa

3) Uhamiaji wamuhoji mdogo wake Niwemugizi

4) Askofu Niwemugizi, asitisha Misa na Ibada zote Jimbo la Rulenge, awataka waumini Wasali Majumbani pia Wajikinge na Corona
 
Nchi tumepitia kipindi kigumu sana....

Kuna kipindi mtu anashitakiwa uchochezi anaenda kupimwa mkojo [emoji16] [emoji16] [emoji16] [emoji16]
[emoji23][emoji23][emoji23],Da umenikimbusha mbali,Nakumbuka hapa ndio Lissu aliwachomesha mahindi mchana kutwa maafande kila wakimwambia tupime anawaambia hampati mkojo wangu hapa, jamaa wakamwachia,ndio akaja kutuelimisha kwamba kisheria polisi hana hayo mamlaka mpaka amri itoke mahakama na hata hivyo unaweza kukataa maana sheria inasema mpaka mhusika 'aridhie' na kusaini.
 
[emoji23][emoji23][emoji23],Da umenikimbusha mbali,Nakumbuka hapa ndio Lissu aliwachomesha mahindi mchana kutwa maafande kila wakimwambia tupime anawaambia hampati mkojo wangu hapa,jamaa wakamwachia,ndio akaja kutuelimisha kwamba kisheria polisi hana hayo mamlaka mpaka amri itoke mahakama na hata hivyo unaweza kukataa maana sheria inasema mpaka mhusika 'aridhie' na kusaini.
Jamaa sheria zote zimekaa kichwani wakaona the only solution ni yeye ku-rest in peace
 
Askofu Niwemugizi alipotumia uhuru wake wa kutoa maoni, kufumba na kufumbua, makachero wakamvaa na kumpora pasi ya kusafiria. Wakauliza, "Wapi kaburi la bibi ya babu yako?"

Sasa kabla Baba Askofu hajaanza ibada ya mazishi, mrudishieni kwanza pasi yake ya kusafiria.

Kwa hiyo Askofu yeye hatokufa? Au yeye atakuwa wa mwisho kufa?
 
Back
Top Bottom