Aliyejifanya Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa ashughulikiwa

Aliyejifanya Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa ashughulikiwa

Kuna unafuu mkubwa kumchokozi mwenye mbwa kuliko kumshika mdomoni mbwa mwenyewe. Huyu kamgusa mbwa ndio maana kang'atwa vilivyo
Kumbuka unaweza ukamchokoza mwenye mbwa na bado akamuamuru mbwa wake akung'ate vile vile
 
Ila Wajita kwa kujifanya much know!! Ngoja akanyee debe!
 
Kweli kakosa ila sio kwenda jela miaka mitano,
Kivyangu naona miezi sita ingetosha
 
Vijana wa hovyo kweli, haya ni madhara ya mtaala wa kijinga. Yaani hata kwa kutumia akili ndogo huwezi kutuma ujumbe kwa kutumia majina ya watu ukijua wewe sio huyo mtu na lazima watu watamtafuta mhusika tu kwa namna yoyote ile.
Maagizo kama hayo labda unge hack namba ya mhusika unayetaka uwe lakini sio huo ujinga.
Ngoja kakakae miaka 5 kakirudi uraiani katakuwa na adabu
 
Tarehe 12/08/2022 RAYMOND NJOFU BWIRE (28) Mkazi wa Kamguluki Mkoa wa Mara alikamatwa na Jeshi la Polisi kwa kosa la kutuma ujumbe mfupi kwenye simu ya mkononi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mlele Mkoani Katavi anayejulikana kwa jina la TERESIA IRAFY

BWIRE alimtaka Mkurugenzi IRAFY kumsaidia mdogo wake kupata kazi ya utendaji wa Kijiji kwa kujitambulisha kwa jina la DIWANI ATHUMANI Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Kufuatia suala hilo Mahakama ya Inyonga iliyopo Wilaya ya Mlele Mkoani wa katavi imemuhukumu BWIRE kifungo cha miaka mitano (5) jela kutokana na kosa hilo.View attachment 2331653

Sent from my SM-A325F using JamiiForums mobile app
kuna watu wanaweza kujilipuwa.!
 
Na yule aliyejifanya anafanya kazi ikulu aliishia wapi maana alitapeli watu wengi sana.
 
Sas yule alieombewa Kaz Yuko API itabid awajibike kwa familia yake huyu kwa sababu Ni yey ndio alikuwa anatafutiwa kazi

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom