#COVID19 Aliyekataa chanjo Marekani aitwa Ikulu kuelimishwa umuhimu wa chanjo lakini Tanzania askofu Gwajima aliitwa Tume ya Maadili kukemewa

Kuna tofauti kubwa kati ya dunia ya kwanza na hii yetu ya third.

Wakati askofu Gwajima akiitwa kwenye tume za maadili za bunge na CCM na kuadhibiwa kwa kuhoji umadhubuti wa chanjo wenzetu kule Marekani ni tofauti kabisa.

Mwanamuziki Minaj baada ya kugomea chanjo kutokana na ushuhuda wa ndugu yake kuvimba korodani baada ya kuchanjwa, Serikali ya nchi yake ya Marekani imemualika Ikulu ili akaelimishwe kwa upana kuhusiana na chanjo ya covid 19.

Mungu ni mwema wakati wote!
UnAjilinganisha na nchi iliyopiga Total lock down, nchi iliyowapa kila kaya mamilioni ya Covid stimulus na nchi yetu tuliyoipokea Covid na drama?

Wana muda hao na pesa

Sisi hata Pesa za madawati hazitoshi

Tukianza kuwaita watu ikulu kujadili the obviou ni upotezaji wa rasilimali tu
 
Mambo ya msingi pia, naelewa uimara huo. Na ndo utofauti uliojitokeza kwa athari za Covid, je udeke kwa sababu ya maelezo hayo tu?

Suala ni katika haohao waafrika bado kuna risk groups.

Nenda kwenye mtandao kasome anti-vaccine groups zilivyowini baadhi ya mataifa hapo kabla na yale ya Africa yakiwemo yalipoacha chanjo za chini ya miaka mitano nini kiliwakuta mfano: Nigeria.

Ya kuambiwa changanya na akili yako.
Unasema huchukui hatua, wewe unaenda kuwaua rafiki, jirani, ndugu na wazazi wako walioko kwenye risks kwa kuwapelekea matatizo.
Think big.
Wapi niliposema sichukui hatua bwashee?!

Kujiridhisha ni muhimu ndio maana chanjo zilikuja milioni 1 waliochanjwa ni 345,000 tu miezi miwili sasa.

Kujiridhisha muhimu bwashee hii dunia imejaa watu kinyume cha matarajio ya wanaoimiliki.
 
Rudi kasome kazi za TMDA ambayo ndiyo yenye mandate kisheria juu ya hilo. Na nimeeleza tangu mwanzo ukaangalie utaratibu ulivyo pale ukitaka kuingiza dawa/chanjo/kifaa tiba chochote wanafanyaje??

Ndio wao wanasimamia chochote ukijuacho ns unachotumia hapa kwetu.

Hizo ndiyo kazi za kila unayosikia ikiitwa FDA kwenye nchi husika na kila nchi ina FDA yake. Ndo maana watakwambia nchi fulani inakubali chanjo fulani, kwa sababu kwa wakati huo wameweza kuifuatilia na kujiridhisha. Baadaye zitaongezwa kwa kadri ya uthibitisho na mahitaji.
 
Kuna tofauti kubwa kati ya dunia ya kwanza na hii yetu ya third.

Wakati askofu Gwajima akiitwa kwenye tume za maadili za bunge na CCM na kuadhibiwa kwa kuhoji umadhubuti wa chanjo wenzetu kule Marekani ni tofauti kabisa.

Mwanamuziki Minaj baada ya kugomea chanjo kutokana na ushuhuda wa ndugu yake kuvimba korodani baada ya kuchanjwa, Serikali ya nchi yake ya Marekani imemualika Ikulu ili akaelimishwe kwa upana kuhusiana na chanjo ya covid 19.

Mungu ni mwema wakati wote!
Nicki Minaj haja alikwa Ikulu. Ameambiwa anaweza kuongea na Ikulu kwa simu, yeye akadai kuwa amealikwa! Serikali ya Trinidad imemtafuta huyo mtu aliyevimba korodani bila mafanikio na hivyo kumshutuma Miss. Minaj kuwa amewapotezea muda kwa kusema uongo.

Pamoja na kusema hivyo, kumkataza Rashidi Gwajima kuzungumzia anacho amini kuhusu COVID-19 sio vizuri. Anatakiwa ajibiwe kwa hoja na sio ubabe.

Amandla...
 
Antivaxxers ni wapuuzi sana

Wazushi na waongo … na sielewi lengo lao nini
 
Nicki Minaj haja alikwa Ikulu. Ameambiwa anaweza kuongea na Ikulu kwa simu, yeye akadai kuwa amealikwa! Serikali ya Trinidad imemtafuta huyo mtu aliyevimba korodani bila mafanikio na hivyo kumshutuma Miss. Minaj kuwa amewapotezea muda kwa kusema uongo.

Pamoja na kusema hivyo, kumkataza Rashidi Gwajima kuzungumzia anacho amini kuhusu COVID-19 sio vizuri. Anatakiwa ajibiwe kwa hoja na sio ubabe.

Amandla...
Kualikwa siyo lazima utimbe physically kama alivyofanya Dr Slaa na Tundu Lisu wakati wa JK.

Hii ni dunia ya digital bwashee!
 
Nicki Minaj haja alikwa Ikulu. Ameambiwa anaweza kuongea na Ikulu kwa simu, yeye akadai kuwa amealikwa! Serikali ya Trinidad imemtafuta huyo mtu aliyevimba korodani bila mafanikio na hivyo kumshutuma Miss. Minaj kuwa amewapotezea muda kwa kusema uongo.

Pamoja na kusema hivyo, kumkataza Rashidi Gwajima kuzungumzia anacho amini kuhusu COVID-19 sio vizuri. Anatakiwa ajibiwe kwa hoja na sio ubabe.

Amandla...

Ongea vitu vinavyoleta maana si kuongea tu, ukiulizwa unayoyasema una ushahidi wa kitaaluma unakosa majibu.

Uhuru huu tuutumie kiungwana. Tuwajibike kwa yale tunayoyapeleka kwenye jamii na tupeleke yenye tija.
 
Shida yako unadhania simu janja hauwezi kuitumia zaidi ya WhatsApp na JF. Badala ya kuniomba mimi ushahidi m Google Nicki Minaj ndio utajua ukweli uko wapi. Msipende kutafuniwa na kulishwa kila kitu.

Hilo la uhuru sikujibu maana hauelewi maana yake.

Amandla...
 
Mwambieni chifu kuna kuvimba nanihii ukichanjwa kama akiuliza tena " mtachanjwa hamchanjwi?".
 
Nadhani hujaelewa nilichoeleza:
Nimesema juu ya maelezo aliyoyatoa Gwajima.

Tutoe maelezo ambayo yana msingi na hoja za kitaaluma. Ni si kwa sababu ti unaamini hivyo basi unaipa jamii unachokiamini hata kama hakina mantiki.

Ndo nikasema watu tutumie uhuru wetu wa kujieleza vizuri jwa kutoa yale yenye kuijenga jamii.
 
Hapo swala ni kuchunguza:
1: Ni kweli ni zao la chanjo?
2: Ni coincidence?

Unaweza kuvimba korodani hata bila kuchanja, tuwe na nafasi ya tafakari na si kwenda na upepo tu. Tafakari hasi vs chanya, tafuta njia mwafaka.
 
Wewe unavimbaga korodani?!
 
Kila nchi na utaratibu wake, utaratibu sio coca cola unachukua tu na kuutumia
 
Nadhani hujaelewa nilichoeleza:
Nimesema juu ya maelezo aliyoyatoa Gwajima.

Tutoe maelezo ambayo yana msingi na hoja za kitaaluma. Ni si kwa sababu ti unaamini hivyo basi unaipa jamii unachokiamini hata kama hakina mantiki.

Ndo nikasema watu tutumie uhuru wetu wa kujieleza vizuri jwa kutoa yale yenye kuijenga jamii.
Bado uko pale pale. Kwa dunia ya leo kumkataza Gwajima kuongea anachoongea ni kufanya watu wazidi kumuamini. Badala ya kumtaka azungumze unavyotaka, muachie aongee na wewe umjibu kwa hoja. Watu wskiendelea kumuamini basi ujue ni fungu la kukosa na hawatakuamini hata useme nini. Yeye anaamini kuwa anachosema ni cha msingi na kina mantik na mashabiki wake wana amini hivyo. Watu ambao waliahidiwa kinu cha umeme, treni ya umeme, boti za kuvua samaki, chuo cha uvuvi, safari kwenda Japan na Marekani, ndugu zao kufufuliwa n.k. lakini bado wanamuona kama Mungu, hata useme nini hawatakuamini dhidi yake. Ni kunawa mikono na kuhangaika na mamilioni ambao wana wasiwasi lakini sio watu wa cult yake.

Amandla...
 
Wewe unavimbaga korodani?!

Unatakiwa uelewe siyo kukariri.
Hoja ni tukio lililotokea kufanyiwa utafiti:
1: kuna watu wengi wanatibiwa matatizo ya kuvimba kirodani na hawajachanjwa.
2: kuna watu wamechanjwa na hawajavimba kirodani.

Hivyo suala ni kutafuta kesi husika:
1: chanjo inahusika?
2: chanjo haihusiki?
3: kama inahusika tatizo liko wapi?
4: kama haihusiki tatizo ni nini?
 
Nimetulia, unaweza kutumia jukwaa hili ukapata maarifa mengi na pia tunaweza kupoteza nafasi za kujifunza tusiyoyajua.
Ujumbe umefika mkuu

You can’t be misleading and a guider at the same time
 
Back
Top Bottom