DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Aliyekuwa diwani wa kata ya Kitangiri wilayani Ilemela jijini Mwanza Donnard Ndaro na kukatwa kwenye mchakato wa kutetea nafasi yake kupitia chama cha mapinduzi CCM ambae kwa hivi sasa anatetea nafasi yake kupitia chama cha ACT wazalendo amewashukuru wananchi wa kata hiyo kwa jitihada za kumtetetea walizoonyesha
Kipindi cha mchakato wa kura za maoni wananchi wa kata hiyo ya kitangiri waliandanamana hadi katika ofisi ya CCM mkoa wa Mwanza wakitaka jina la mgombea huyo lirudishwe wakidai ndiyo chaguo lao huku waraka wa chama hicho Taifa ukielekeza walioenguliwa kurudishwa na kupigiwa kura jambo ambalo katika kata hiyo lilishindikana kufanyika
Aidha baada ya jitihada za wananchi hao kugonga mwamba ndipo mgombea huyo Donnard Ndaro akatimkia chama cha ACT wazalendo na kuamua kutetea kiti chake cha udiwani na wakati akizindua kampeni zake akaamua kuwashukuru wananchi hao kwa kuonyesha upendo kwake huku akiwaahidi kuwatumikia kwa uaminifu mkubwa.