Aliyekubali Switch za bwawa la umeme la Rusumo Tanzania zikawekwe Rwanda ametumia akili zake ipasavyo?

Nimepata taarifa zisizo rasmi kwamba eti lile bwawa la umeme la Rusumo linalojengwa huko Ngara Tanzania, eti switch zake za kuwashia na kusambazi umeme zinafungwa Rwanda.

Maana yake ni kwamba Tanzania itakuwa ikizalisha umeme, halafu huo umeme utasafiri hadi Rwanda, halafu Rwanda ndio itakua inawasha hizo Switch ili kuruhusu umeme uje Tanzania.

Je, kuna mantiki yeyote juu ya maamuzi kama haya? , kwahiyo siku tukipandisha ushuru bandarini kwa mizigo inayoenda Rwanda na wao wanatuzimia switch za umeme hadi tushike adabu, na umeme tunauzalisha wenyewe? Sasa nashangaa, Tanzania tulikosa pesa ya kununulia switch hadi kwenda kuomba mchango wa Rwanda na tugawane nao umeme nusu kwa nusu eti?

Mi nadhani kuwe na haja ya kupimana magonjwa ya akili kabla ya kupeana hizi wizara nyeti hasa za Nishati na madini.., video ina maelezo ya ziada

==========================
Update: 23/04/2023
Wenyewe wanajinadi kimataifa kwamba ni mradi wa Rwanda

Wateule wa Rais hao walio amua hayo na wanayo Jana na ccm
 
Nimeiona hofu tuu ya mtoa mada na sio kitu kibaya. Miradi kama hii inaendeshwa MoU (Memorandum of understanding) baina ya nchi washirika. Na huu mradi upo katika mfumo wa Kampuni ya kibiashara nchi washirika kwa share sawa wameunda kampuni ya kibiashara inaitwa Rusumo Power Plant Limited na ndicho chombo kitakachoendesha mradi na sio nchi husika. Usifikiri kwamba swichi kuwa Rwanda basi zipo Urugwiro Village kwa Kagame na kwamba akijisikia kuzima anazima,maeneo yote yaliyofikwa na mradi ni mali ya kampuni zikiwemo miundombinu. Kampuni hiyo ina bodi kwa uwakilishi sawa kwa uwiano waliopatana na trustee. Naamini wataalamu na wafanyakazi wapo chini ya Bodi husika. Hiyo kusema kwamba tukihitilafiana na Rwanda wazime switch zetu kule kama figisu ili tukose umeme hicho kitu hakiwezi kuwepo.
Pili umeme ni product ya mwisho ya mradi na umeme huo kila nchi ina mgao wa Megawatt (MW) 27 kutoka 80 kila huyu kwenye gridi yake kulingana na mkataba.
Kuhusu swichi kuwa Rwanda inaweza kuwa ni makubaliano ya fursa sawa kimiundombinu yaani "Win win" na sidhani kama zinaathari katika kuendesha mradi husika na mgao au kutumika kuleta figisu figisu za kidiplomasia kama hofu ya wengi ilivyo kuhusu Rwanda.
Mwisho ni kwamba tunahitaji umeme kwa watu wetu.
 
Asilimia kubwa ya Bwawa la Kikagati linajaza maji Tanzania, ila tukitaka umeme tununue!!

Yxzd ZDS,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yani bro trust me nchi hii inaongozwa na watu ambao sio asiliyao hapa ,
Wamezariwa hapa ila wazazi wao sio asili yao hapa.
Hata Magu naye Baba yake alikuwa mrundi.
 
Mda kama huu hawa mende ilikuwa ni kuwakatia umeme tu, hadi washike adabu
 
Back
Top Bottom