Aliyekuwa akiombea Raila Odinga afe aanza kutangulia kufa Yeye huko Nairobi

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Kuna siku moja wakati nikipitia pitia maandiko matakatifu ya katika Biblia niliwahi kuona mahala fulani Mtakatifu Paulo akiwahimiza sana Wakristo hasa juu ya matumizi ya Ulimi na nakumbuka mara kwa mara alikuwa akisema kwamba Ulimi huu huu unaweza kukusababishia matatizo makubwa na kwamba usipokuwa nao makini Ulimi huo huo utakuponza.

Hatimaye Injili ya Mtakatifu Paulo kwa Wakorinto juu ya matumizi ya Ulimi imetimia hivi leo tu baada ya Gavana wa Nyeri Bwana Wahome Gakuru ambaye kwa wiki moja tu au mbili zilizopita alisikika na hadi kununuliwa na Vyomba vya habari vya nchini Kenya akisema kwamba anatamani sana Kiongozi wa NASA sasa NRM Resist Bwana Raila Odinga apigwe risasi afe kwani anaichafua Kenya na hana faida kwa Wakenya.

Kwa bahati mbaya sijui nzuri maombi yake yametimia baada ya Yeye mwenyewe Gavana Wahome Gakuru kufariki dunia kwa ajali mbaya mno ya Gari ambayo ilipasuka tairi yake na ikapinduka vibaya sana wakati wakielekea jijini Nairobi huku Mlinzi wake na Dereva wake nao wakiwa wamejeruhiwa vibaya sana na hali zao inasemekana bado ni mbaya.

Kweli haya ni maajabu ya kweli yaani yule anayeombea mwenzake afe ' mara paaap ' Yeye ndiyo anatangulia Kufa tena Kifo kibaya pengine ni tofauti na ambacho labda atakuja kufa nacho yule aliyekuwa akimuombea afe. Jamani tujitahidi mno kutumia Ulimi kwa kutoa maneno yenye kheri vinginevyo tu maombi yako mabaya kwa GENTAMYCINE yatakufanya Wewe ndiyo utaabike bure kwa mateso halafu Yeye bado anapeta tu kwa nguvu na baraka zake Mwenyezi Mungu.

Naamini kabisa tena kwa 100% kwamba ' message sent and delivered '.

Nawasilisha.
 
Na wewe usichekelee kifo cha mwenzako.

Ila ulitaka nichekelee pale alipokuwa akiombea Raila Odinga afe tena mbele za Waandishi wa Habari wa Kenya? Usinitibue tafadhali mapema yote hii sawa? Unaona post yangu huipendi au haijakupendeza au inakukereketa achana nayo na tembelea posts zingine kwani kuna threads nyingi sana humu JamiiForums.

Halafu kuna kitu huwa nakishangaa na najiulizaga sana kwamba inakuwaje asilimia kubwa ya Watu wanaochukizwa na posts au threads zangu humu JF ndiyo hao hao ambayo kila siku iendayo kwa Mungu lazima tu watazipitia na wakati mwingine hata kuchangia? Najua hapa katika Keyboard mtaonyesha kuchukizwa nami ila najua fika kwamba mioyoni mwenu mnanikubali ile mbaya.

Huwezi ukawa ' Purely Talented and Charismatic Fella ' halafu usijae mioyoni mwa Watu. Kuna Watu Mwenyezi Mungu kawabariki ila kuna wachache wetu tumetunikiwa nae ile Shani / Nyota hivyo hatushangai sana. Naamini kabisa kwamba ' message sent and delivered ' kwa Wanafiki wote wahusika, wanaojijua na wale ambao watajihisi vile vile.
 
Muujiza kama huo ilitokea sana hapa kwetu tena sio muujiza mmoja ni kama saba kama sikosei.....Mzee wa Panya yeye alipewa karipio kali kwa kunusurika na ajali hahahahah...Mungu hataniwi mwambieni yule aliyesema dunia sio ya Mungu eti ni yake na kimungu chake
 
 
hapo umedanganya aliyesema ivo ni Wambugu NGUJIRI mbunge wa nyeri town wala c gavana wa nyeri
 
Weka hiyo clip akimuombea Raila afe...

Otherwise...

Blah blah blahh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…