Aliyekuwa askofu Konde aondolewa wakfu. Fimbo, msalaba na pete yake vyaondolewa wakfu pia. Sasa atabakia kuwa muumini wa kawaida

Aliyekuwa askofu Konde aondolewa wakfu. Fimbo, msalaba na pete yake vyaondolewa wakfu pia. Sasa atabakia kuwa muumini wa kawaida

Ukitaka kulielewa hili vizuri ni kama Magufuli alivyomuondowa CAG Profesa Assad wakati hakuwa na mamlaka hayo kikatiba.

Hivyo basi Askofu wa mnyororo akishawekwa wakfu hakuna mwenye uwezo wa kumvuwa huo Uaskofu hilo halipo.

Kinachowezekana ni kumvuwa tu madaraka ya Kiaskofu kwenye dayosisi na mfano mzuri ni Askofu Mokiwa wa Anglican alivuliwa madaraka tu lakini bado ni Askofu.

Huwezi kumvuwa Jaji title yake, huwezi kumvuwa mwalimu tittle yake, kinachoendelea Konde ni bangi tu kuzidi kutuamsha kwamba dini ni biashara na hii ni vita ya kimaslahi.
CAG muda wake uliisha then hakuongezewa. Siyo lazima muda wa CAG wa kuhudumu ukiisha lazima tema aongezewe.
 
Kutoka ASKOFU hadi kuwa Muumini, tena wa kawaida. Aisee!! Hapana. Hii ni Adhabu kali sana. Mimi ningehama Mji kabisa.

Kuna 'kitu' hakiko sawa katika Uongozi wa KKKT.
sio hakiko sawa mkuu, kuna kitu kinaitwa utii katika kanisa, hicho mapadre wa kiroma wanakijua vyema ,waliosoma seminari, wanajua ni amri moja kama jeshini, sasa kkkt kuna uliberali
 
Kesi kutambua uwepo wa mungu hiyo ni facts ama opinion ya Judges?

Kuna Judges opinion na facts, facts hua zinaletwa mahakamani kama exhibits ama evidences, mungu alietwa mahakamani?
Opinion iliotengeneza principle inayotumika dunia nzima sio...😀😀😀 hio opinion ili supersede facts...
 
Kutoka ASKOFU hadi kuwa Muumini, tena wa kawaida. Aisee!! Hapana. Hii ni Adhabu kali sana. Mimi ningehama Mji kabisa.

Kuna 'kitu' hakiko sawa katika Uongozi wa KKKT.
Haya mambo yapo. Nashauri atulie aanze upya na Mungu.
Haya mengine ni taratibu za kibinadamu tu.
 
Ila Papa hana huwezo wa kumvua Mtumishi wakfu, wanaamini ni MUNGU pekee. Ndiyo maana Mtumishi akikengeuka atatupwa jela ama Segerea au Vatican akimaliza kifungo anahamishiwa Japan au US nk, wakfu wake unaendelea hadi mauti. RC muumini hawezi kumpiga Mtumishi au kumfukuza Parokia, KKKT hiyo ni rampant!
Nani kakudanganya mkuu! Hebu uliza walioleta maada za kuoa wako wapi muda huu.
 
Personally huu mgogoro umenisikitisha sana, kilichohitajika ni hekima ya Mungu ambayo mwaikali na wenzake waliikosa..

yeye ambaye tuliamini ni mpakwa mafuta baada ya matatizo yote tulidhania ange kaa na kusali na kuachia kwa amani kanisa libaki na umoja na Mungu amtetee wabaya waonekane, cha ajabu kaanzisha kizungumkuti cha ajabu, Mungu hajawahi muacha mjawa wake I guess faith yake ilititirika kidogo, Mungu amsaidie
 
Ila Papa hana huwezo wa kumvua Mtumishi wakfu, wanaamini ni MUNGU pekee. Ndiyo maana Mtumishi akikengeuka atatupwa jela ama Segerea au Vatican akimaliza kifungo anahamishiwa Japan au US nk, wakfu wake unaendelea hadi mauti. RC muumini hawezi kumpiga Mtumishi au kumfukuza Parokia, KKKT hiyo ni rampant!

Sio kweli kuna Paddre mmoja kule ukelewe alikataa mtu asiungame mbele yake akasema yeye sio Mungu taarifa zilipelekwa kwa askofu ,askofu akazituma kwa Papa ,Papa akasema huyo Padre anatakiwa aondolewe kwenye upadre halafu afukuzwe dhehebu la roman catholic
 
Tupe kajistor MBNA una ambaa juu juu tu.
Kastori Kako hivi, inasemekana pale Mji Mpya, kulikuwa na ujenzi wa kanisa uliochukua muda mrefu kukamilika. Ucheleweshaji huo ulikuwa ni mpango wa 'wasimamizi wa ujenzi' kufaidi matoleo ya waumini bila idhini(umenielewa nadhani). Sasa Mchungaji mpya akaletwa, alikuwa amenyooka kama rula, kama ni nyeupe anasema ni nyeupe na kama ni nyeusi anasema ni nyeusi! Kwa muda mfupi Kanisa likajengwa kwa Kasi na likawa katika Hali ya kukamilika. Mchungaji akawa mfuatiliaji mzuri wa sadaka ya mavuno. Mchungaji akaanzisha huduma za afya kwa waumini kwa kutumia waumini wenye taaluma hiyo hapo kanisani. Hata elimu ya ujasiliamali ikawa inapenyezwa kwa waumini.

Kwa chini chini, inasemwa Mchungaji alikuwa anaamini kanisa litaimarika kwa kuwa na waumini wenye afya njema na elimu ya sahihi ya kujipatia kipato kwa haki.
Kweli kanisa likaimarika. Waumini wakafurika, Kila jumapili sadaka za kutosha. Seminar mbalimbali za vijana na wenye ndoa zikashamiri pale. Akawezesha vijana wa kike na kiume kuolewa na kuoa hapo kanisani. Mchungaji akanunuliwa gari kwa haki. Aisee, shetani naye akajikita kiwanjani, wale walibaniwa kukwamishwa ujenzi' wa kanisa wakajiimarisha. Wale wakashirikiana na baadhi ya simamizi wa dayosisi wasielewa umuhimu wa haki wakaanzisha zengwe! Mchungaji akahamishwa kutoka usharikani hapo akapelekwa kwingine! Dayosisi ikapata msukosuko!

Hao waliratibu vurugu kwa Mchungaji wakagundulika wakavuliwa mamlaka! Karma ya Paskali wa JF ikafanya kazi.

Ni hayo niliyonasa kwenye mtaa!
 
Hawa jamaa wakizinguana inakuwa burdani sana vile vifaa vya bendi ndo vinageuzwa kuwa silaha. Mzeiya umekaa kihasarahasara unakula gitaa matata la kiuno🤣🤣
Badala ya gitaa kucharazwa lenyewe ndiyo linacharaza kiuno cha mtu. Teeh teeh.
 
Kanisa la KKKT Dayosisi ya Konde leo imetangaza kumwondolea wakfu wa Uaskofu aliyekuwa askofu wa Dayosisi hiyo, Dk. Edward Mwaikali.

Pia imeviondolea wakfu vifaa vya Kiaskofu alivyokuwa anatumia kama pete, msalaba pamoja na fimbo ambavyo alikabidhiwa tarehe 18 Januari 2018 alipowekwa wakfu kuiongoza Dayosisi ya Konde.

Uamuzi huo umefanyika leo Jumapili Juni 5, 2022 wakati wa lbada ya kumweka wakfu mrithi wake, Dk. Geofrey Mwakihaba.

Wamefikia hatua hiyo baada ya Dk. Mwaikali kugoma kuvirejesha ili vitumike kwa mrithi wake kwa mujibu wa taratibu za kanisa hilo.

Dk. Mwaikali aliondolewa madarakani tarehe 22 Machi 2022 na Mkutano Mkuu Maalum wa KKKT Dayosisi hiyo kwa kile kilichoelezwa kushindwa kuiongoza vyema.

Vitu vingine ambavyo amegoma kuvirejesha ni kiti cha uaskofu na mavazi ambavyo navyo vimeondolewa wakfu.

View attachment 2251168
Mimi nauliza tu,hiyo misalaba pete na fimbo ,warilithi kutoka kwa nani?
 
Kazitema hela kiboya sana Mwaikali
Kifupi Mwaikali ni mpagani aliyeupata uaskofu kwa kuhonga wajumbe wa mkutano mkuu.Ni mpagani kabisa hana cha U KKKT kama mpagani Jerry Mngwamba aliyekuwa Askofu wa Dayosisi ya mashariki na Pwani
 
Kwa hiyo hicho kidegree chako cha sheria ndo unajiona umesoma! Wakati umekariri historia tu huna hata uwezo wa kuziba pancha ya baiskeli! Eti sheria stupid sheria gani unaitumikia wakati asilimia zaidi ya 90 mmeutoa kwenye vitabu vya dini! Nyinyi mnajiita wanasheria wasomi wakati mmejaa upumbavu kichwani!
 
Mimi sio muumini wa dini kwa sababu mungu hayupo ila dini kama taasisi za kihiyari zina taratibu zake na lazima kama unataka kua muumini ama kiongozi ufuate hizo taratibu.

Huyo askofu alienda kinyume na taratibu za kanisa na kujiona ni mkubwa kuliko kanisa sasa kanisa limemmaliza kabisa.

Ni vyema watu kuheshimu taratibu za taasisi walizokubali kwa hiyari yao kua wanachama ama viongozi.

Nakumbuka miaka ile ya kuibuka kwa makanisa ya kilokole, kiongozi mmoja wa kanisa la kilokole, Kulola aliasi TAG na akaamua kukatalia majengo na makanisa ya TAG. Tukawa tunajiuliza kama umeamua kua mwenyewe kivyako si uachie vitu vya watu, ikawa shida kubwa.

The same ikaja kwa Free Pentecoste church na Pentecoste church of Tanzania, Mlima wa Moto(Juzi nimesikia mchungaji wa mlima wa moto amefichwa tabata na changudoa toka mwezi wa 2, hii ni balaatupu mchungaji kutekeleza kondoo aliopewa awaongoze amejificha kwa malaya anakula utamu tu) na TAG, Father Nkwere na Kanisa Katoliki nk.
kama jambo ulijuh kaa kimya
 
Ni nini wameamua kumdhihaki hivi.

Wameshindwa kumstahi hata kidogo mpaka wanamdhalilisha hivi.

Hivi vitu unaweza ona ni kawaida ila vinaumiza moyo.

Wao wana uhakika upi kuwa ni watumishi halali wa Bwana.
sasa na yeye kwanini Agombanie uwongozi ?
Huko ni kupigana vita ya Mungu, kama watu hawakutaki unaachana nao.
 
Back
Top Bottom