Aliyekuwa askofu Konde aondolewa wakfu. Fimbo, msalaba na pete yake vyaondolewa wakfu pia. Sasa atabakia kuwa muumini wa kawaida

Aliyekuwa askofu Konde aondolewa wakfu. Fimbo, msalaba na pete yake vyaondolewa wakfu pia. Sasa atabakia kuwa muumini wa kawaida

Kuna 'kitu' hakiko sawa katika Uongozi wa KKKT.
Walimvurugia Mchungaji mmoja mwaminifu kweli ambaye alikuwa anawawezesha waumini kuona thamani ya sadaka zao pale Mji Mpya Morogoro, ikaniuma sana, lakini Karma ya 'Paskali wa JF' ikawashughulikia waliofanya uhuni huo.
 
Hawa RC sio kama hawana mauozo yao kama hawa wengine ni vile tu wao hawajaruhusu demokrasia (unasali unasepa zako hakuna maswali sijui sadaka au uongozi unafanya nini sijui) ndomaana uezi kusikia chochote lakini ukitaka kujua wakoje ww kaa na watu wa uko ndani malalamiko yapo kibao tu ila ndoivo yanaenda kichinichini hutayasikia kamwe
Ila Papa hana huwezo wa kumvua Mtumishi wakfu, wanaamini ni MUNGU pekee. Ndiyo maana Mtumishi akikengeuka atatupwa jela ama Segerea au Vatican akimaliza kifungo anahamishiwa Japan au US nk, wakfu wake unaendelea hadi mauti. RC muumini hawezi kumpiga Mtumishi au kumfukuza Parokia, KKKT hiyo ni rampant!
 
Walimvurugia Mchungaji mmoja mwaminifu kweli ambaye alikuwa anawawezesha waumini kuona thamani ya sadaka zao pale Mji Mpya Morogoro, ikaniuma sana, lakini Karma ya 'Paskali wa JF' ikawashughulikia waliofanya uhuni huo.
Basi ndiyo maana. Karma is a bitch.
 
KKK (T) inachekesha sana hapa duniani.

Maswali wsiyoweza kujibu:

1. Wakfu huwa ni wa binadamu au MUNGU?

2. Kwanini Kanisa lina madeni yasiyolipika kama ya HIPC?

3. Kwanini Maaskofu hawawezi kuhamishwa Dayosisi? (Wako autonomous)

4. Kwanini Watumishi wanakosaga mishahara wakati fulani na mara nyingi?

5. Kwanini Maaskofu wengine wana muda maalum wa kutumika na wengine wanakaa hadi kustaafu kwa Kanisa hilo hilo moja?

6. Kama Kanisa limewekeza kwenye elimu kuanzia shule za awali hadi vyuo vikuu kwanini watoto wa watumishi wanafukuzwa kwa kukosa ada? Utumishi wa wazazi wao hautoshi kuwa dhamana ya kusoma bila ada? (kwanini wasipewe scholarship?)

7. Kama Kanisa limewekeza kwenye afya kuanzia afya ya msingi hadi ya umma (Primary to Public Health) kwa maana ya zahanati, vituo vya afya, hospitali, hospitali teule, hospitali za rufaa, hospitali za umahiri (consultant hospitals) kwanini watumishi na familia zao wafe kwa kukosa ela za medical evacuation kwenda ughaibuni? Kwanini wanakuwa ombaomba kwa ndugu, jamaa, marafiki, majirani, waumini ndiyo wawachangie?

8. Kwanini watumishi wanaoondolewa wakfu wakienda wakaanzisha Makanisa yao au Huduma zao wanafanikiwa sana? Wakfu huwa ni wa binadamu au MUNGU? Angalia Mwingira alikuwa Mwinjilisti wa KKKT, angalia Fernandes alikuwa Mchungaji wa Pentecost, angalia Moses Kulola alitimuliwa TAG akaanzisha EAGT nk nk.

9. Kwanini asilimia 90 ya watumishi kwenye Makanisa haya ya Kimagharibi wanafanikiwa kiuchumi nje ya mfumo wanaouhubiri? Wakianzisha na kusimama kwenye Makanisa yao au Huduma zao ndipo wanapopata mafanikio makubwa na kuwa Mamilionea. Mwingira aliitangulia KKKT kuanzisha benki, Tv, Kilimo na Ufugaji Katavi, Sacoss, mgodi Arusha nk. Fernandes pia aliitangulian Pentecost kuanzisha Tv.

10. Kwanini watumishi wanaotumika kwenye vituo vya Dayosisi (siyo Dayosisi kwenyewe) baadhi yao wana ugomvi wa sadaka na waumini?

Hapo juu namba 4, 6, 7, 9 na 10 wahanga wake ni watumishi walio chini kwenye vituo vya Dayosisi, siyo walio makao makuu ya Dayosisi.
Mkuu kufanikiwa kwa kupata wafuasi ama kupata Mali nyingi hakuna uhusiano na kuupata uzima wa milele.

Mungu ametuacha huru hapa Duniani na uchaguzi wetu.
 
Hawa jamaa wakizinguana inakuwa burdani sana vile vifaa vya bendi ndo vinageuzwa kuwa silaha. Mzeiya umekaa kihasarahasara unakula gitaa matata la kiuno🤣🤣
 
Hakuna lililo kwisha msidanganyike Mungu hadhihakiwi
Kweli kabisa mkuu,

Wapentekoste walifikiri Gamanya ndiye tatizo kumbe siyo.

Gamanywa alianzisha redio kwa kutumia mitambo ya Pentecost, Wapentekoste wakamzulia ugomvi kwamba redio ni yao, kumbe hawakujuwa redio siyo mitambo ambayo ndiyo ilikuwa yao, huku Gamanywa akimiliki leseni na masafa, ndiyo wakaja kujuwa kwamba kumbe redio ni leseni na masafa, siyo mitambo na news room.
 
Mkuu hauifahamu RC wewe. Hao mapadri ni mamilionea wenye familia za kujificha. Kuna ambaye anafahamika maeneo ya mwenge hapa dar.
Pia uaminifu wao je kuhusu kuwachakata watoto wadogo vip hyo
 
Niseme tu kuw wanyakyusa Ni wafurugaji Sana

Ingawaa bwana mwaikali alikuwa sahihi kuamua kutoa makao makuu ya dayoss kuamishia mjini center ambapo kila mtu aliweza kuaccess kuliko ilivyo kuwa huko tukuyu

Labda alifanya hvyo kwa ubabe Bila baraka za mkuu wa kanisa hili ambaye Ni baba asko Dr Fred shoo
 
Kwa sababu hawajaoa; kama wangekuwa na wake, haya matatizo yangewakuta
Ni kweli ndiyo maana baadhi ya Manabii na Mitume waliofanikiwa sana nyakati zao hawakuoa. Musa naye aliamua kuchukuwa mke na watoto akamrudishia babamkwe wake mzee Yethro kuwa awamiliki milele ili yeye abaki huru kufanya kazi ya Mungu. Paulo Mtume naye hakuoa kwa sababu hizo hizo. Yesu Kristo (kama mtu siyo kama Mungu) ambaye ni Nabii wa mwisho na Mtume wa kwanza hakuoa pia.
 
Back
Top Bottom