Aliyekuwa askofu Konde aondolewa wakfu. Fimbo, msalaba na pete yake vyaondolewa wakfu pia. Sasa atabakia kuwa muumini wa kawaida

Aliyekuwa askofu Konde aondolewa wakfu. Fimbo, msalaba na pete yake vyaondolewa wakfu pia. Sasa atabakia kuwa muumini wa kawaida

Kamuulize huyo Askofu Mwaikali kama havina mchango wowote kwa nini kagoma kuvirudisha
Akitaka kutest kama wakfu umeondoka au la mwambie ajaribu kuitisha mkutano mkubwa wa nje wa injili pale Mbeya Mjini muone hilo nyomi.
 
Aligonga mkenge mahakamani jana, Mahakama ya Kanda ya Mbeya!
Waliompeleka Mahakamani nadhani wamevunja Katiba ya Dayosisi. Katiba nyingi za KKKT zinazuia masuala ya Kikanisa kupelekwa Mahakamani. Km Katiba yao pia inasema hivyo, basi waliompeleka Mahakamani wamevunja Katiba hivyo na wao inabidi waonyeshwe mlango wa kutokea.
 
Akitaka kutest kama wakfu umeondoka au la mwambie ajaribu kuitisha mkutano mkubwa wa nje wa injili pale Mbeya Mjini muone hilo nyomi.
Mwaikali na kuhubiri mikutano ya injini wapi na wapi.Yule alikuwa Askofu wa mambo ya miradi na pesa hana cha mikutano ya injili wala nini yule.
 
Walimvurugia Mchungaji mmoja mwaminifu kweli ambaye alikuwa anawawezesha waumini kuona thamani ya sadaka zao pale Mji Mpya Morogoro, ikaniuma sana, lakini Karma ya 'Paskali wa JF' ikawashughulikia waliofanya uhuni huo.
Tupe kajistor MBNA una ambaa juu juu tu.
 
Mwaikali na kuhubiri mikutano ya injini wapi na wapi.Yule alikuwa Askofu wa mambo ya miradi na pesa hana cha mikutano ya injili wala nini yule.
Mob Psychology haiangalii unajuwa au hujui kuhubiri, ni kilichokukuta (agenda iliyoko kwenye spotlight) ndiyo inayovuta umati wa watu na wafuasi.
 
Mwaikali hana mvuto wa kiinjili
Hata mvuto tu wa Uaskofu hana alipewa tu kwa ufisadi tu na rushwa
Musa hakustahili Unabii? Kwanini Mungu hakumpa Haruni aliyekuwa fundi wa kuongea kwa ushawishi?

Mbona ni Musa huyo huyo asiyeweza kushawishi (mwenye kithembe na kigugumizi kikali) ndiye aliyepindua serikali ya Misri iliyoongozwa na Farao wa 40?

Kuchagua Maaskofu huwa sura zinaangaliwa kama kigezo na sifa? Uchaguzi wa Askofu siyo mashindano ya ulimbwende.

Daudi alistahili utumishi/ufalme kuliko nduguze? Alikuwa na mvuto?
 
Wewe mburula, hizo ni taarifa zinapatikana kwenye public domains. Wengine sisi ni wanasheria tumehusika kwenye cases nyingi ya taasisi mbalimbali zikiwemo za dini hivyo tunajua.

Una akili ndogo sio rahisi kuelewa mambo mengi kwa wakati mmoja.
Watu bhana...kielimu kidogo tu..Mungu hayupo...mnasikitisha sana.
 
Ni nini wameamua kumdhihaki hivi.

Wameshindwa kumstahi hata kidogo mpaka wanamdhalilisha hivi.

Hivi vitu unaweza ona ni kawaida ila vinaumiza moyo.

Wao wana uhakika upi kuwa ni watumishi halali wa Bwana.
We wa mlimani na wewe ni mKKKT sio? Kule hakuna ya rohoni kule kuna ya meilini ni biashara tu. Uaskofu wa kupewa na watu utanyang'anywa na watu. Kinachotakiwa ni uaskofu ule wa kupewa na Mungu. Huo hakuna mwanadamu anayeweza kukuondolea.

YESU KRISTO NI BWANA NA MWOKOZI
 
Tunamkaribisha hapa jangwani tunawapokea waumini waliokataliwa kwenye madhehebu yao feel free church.
 
Wewe mburula, hizo ni taarifa zinapatikana kwenye public domains. Wengine sisi ni wanasheria tumehusika kwenye cases nyingi ya taasisi mbalimbali zikiwemo za dini hivyo tunajua.

Una akili ndogo sio rahisi kuelewa mambo mengi kwa wakati mmoja.
Kuwa mburula siyo tatizo kwa sababu fani yo yote isiyo yako utakuwa mburula kwenye hiyo fani may be huyo hayupo kwenye masuala yanayoweza mpa hizo taarifa.Yaani ni sawa na wewe ulivyo mburula kwenye elimu inayomhusu Mungu ndo maana umburula huo unakupa hitimisho hakuna Mungu, ilhali wenye ufahamu na elimu kumhusu Mungu tuna uhakika yupo,alikuwepo na milele atadumu kuwepo.

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Musa hakustahili Unabii? Kwanini Mungu hakumpa Haruni aliyekuwa fundi wa kuongea kwa ushawishi?

Mbona ni Musa huyo huyo asiyeweza kushawishi (mwenye kithembe na kigugumizi kikali) ndiye aliyepindua serikali ya Misri iliyoongozwa na Farao wa 40?

Kuchagua Maaskofu huwa sura zinaangaliwa kama kigezo na sifa?
Musa alikuwa mtu wa vitendo sio maneno alifanya miujiza kibao bila kelele wala Maneno ndivyo vilimtikisa Farao .Farao hakutikiswa na hotuba nzuri na maneno yaliyopangiliwa vizuri kisomi na kitheolojia ya Haruni!!

Mwaikali usimfananishe na Musa

Mwaikali hata miujiza haamini kuwa ipo siku za leo kifupi yeye imani yake imejikita kuwa kanisa ni Generator la ku generate pesa tu mambo ya kiroho kwake yako mbali naye
 
We wa mlimani na wewe ni mKKKT sio? Kule hakuna ya rohoni kule kuna ya meilini ni biashara tu. Uaskofu wa kupewa na watu utanyang'anywa na watu. Kinachotakiwa ni uaskofu ule wa kupewa na Mungu. Huo hakuna mwanadamu anayeweza kukuondolea.

YESU KRISTO NI BWANA NA MWOKOZI
Na Bagonza je? Hiyo ndiyo KKKT yetu!
 
Musa alikuwa mtu wa vitendo sio maneno alifanya miujiza kibao bila kelele wala Maneno ndivyo vilimtikisa Farao .Farao hakutikiswa na hotuba nzuri na maneno yaliyopangiliwa vizuri kisomi na kitheolojia ya Haruni!!

Mwaikali usimfananishe na Musa

Mwaikali hata miujiza haamini kuwa ipo siku za leo kifupi yeye imani yake imejikita kuwa kanisa ni Generator la ku generate pesa tu mambo ya kiroho kwake yako mbali naye
Paulo alianza hivyo hivyo kama Mwaikali, akalitesa Kanisa na kuua Watumishi wenye kibali. Sasa yeye ndiye amejaza Biblia kwa Nyaraka (13) kuliko waliokuwa na upako na utakatifu tangu mwanzo. Haya yaliyomkuta Mwaikali yanamtafakarisha upya kwenye wito wa Mungu. Usihukumu leo yangu angalia kesho yangu, Mungu anaangalia mwisho wa mtu au jambo siyo mwanzo.
 
Waliompeleka Mahakamani nadhani wamevunja Katiba ya Dayosisi. Katiba nyingi za KKKT zinazuia masuala ya Kikanisa kupelekwa Mahakamani. Km Katiba yao pia inasema hivyo, basi waliompeleka Mahakamani wamevunja Katiba hivyo na wao inabidi waonyeshwe mlango wa kutokea.
Yeye mwenyewe ndo alikimbilia mahakamani kugoma asitoke kwenye nafasi yake, na huko alikokimbilia bado amedondokea pua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Paulo alianza hivyo hivyo kama Mwaikali, akalitesa Kanisa na kuua Watumishi wenye kibali. Sasa yeye ndiye amejaza Biblia kwa Nyaraka (13) kuliko waliokuwa na upako na utakatifu tangu mwanzo. Haya yaliyomkuta yanamtafakarisha upya kwenye wito wa Mungu. Usihukumu leo yangu angalia kesho yangu, Mungu anaangalia mwisho wa mtu au jambo siyo mwanzo.
Wakati Paulo akilitesa kanisa hakuwa Mkristo alipobadilika kuwa Mkristo ndio akawa vizuri sana

Mwaikali katesa kanisa akiwa Mkristo
Usimlinganishe na Paulo!!
 
Back
Top Bottom