Aliyekuwa jenerali wa jeshi la Uganda UPDF Peter Elwelu akamatwa

Aliyekuwa jenerali wa jeshi la Uganda UPDF Peter Elwelu akamatwa

carbohydates

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2026
Posts
260
Reaction score
607
Aliyekuwa Jenerali wa Jeshi la Ulinzi la Uganda (UPDF), Peter Elwelu, anadaiwa kukamatwa na Vyombo vya Usalama katika Mji wa Soroti, jioni ya Jumatatu, Novemba 2, 2026.

Taarifa za kukamatwa kwake zinafuatia msako uliofanyika hivi karibuni katika mojawapo ya makazi yake, ambapo Vyombo vya Usalama vinadaiwa kukuta Bunduki 15, sare za Kijeshi pamoja na Magari mawili aina ya Pick-up.

Elwelu, ambaye alistaafu Jeshi takribani miaka miwili iliyopita, amekuwa akiikosoa Serikali ya Uganda, hususan kuhusu masuala ya rushwa. Ukosoaji huo unadaiwa kumuweka katika mgogoro na baadhi ya Viongozi wa Serikali na Jeshi, akiwemo Mkuu wa Majeshi, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, ambaye kwa mujibu wa taarifa hizo aliagiza atafutwe.

Peter Elwelu pia ni miongoni mwa maafisa wa Kijeshi waliowekewa vikwazo na Marekani kutokana na tuhuma za kuhusika na ukiukwaji wa haki za binadamu.

Vikwazo hivyo vinahusishwa na matukio ya umwagaji damu yaliyotokea katika Ufalme wa Obusinga Bwa Rwenzururu, ambako watu waliuawa wakati wa Operesheni za Vyombo vya usalama.

===============
Retired Lieutenant General Peter Elwelu has been arrested by security forces in Soroti City over alleged involvement in subversive activities and plans to destabilise the Teso sub-region, the UPDF has said.

In a statement issued on Monday evening, UPDF Acting Spokesperson Col Chris Magezi said Elwelu had been on the run before his arrest.

"Renegade UPDF Officer Peter Elwelu has this evening been arrested by security forces in Soroti City. He has been on the run over involvement in subversive activities and plans to destabilize Teso," Col Magezi said.
Magezi further claimed that security forces had recently recovered 15 guns, military fatigues and two pickup trucks allegedly linked to Elwelu.

"The security forces recently recovered 15 guns in his possession, military fatigues, and two pickup trucks," he said.
The army spokesperson said Elwelu would be charged and prosecuted in accordance with the law.
"He will be charged and prosecuted in the courts of law accordingly," Col Magezi said.

Elwelu, who retired from active military service with the rank of Lieutenant General, previously served as Deputy Chief of Defence Forces and Commander of the UPDF Land Forces.
By press time, details surrounding the circumstances of his arrest and when he would be produced in court remained scanty.
 
Back
Top Bottom