Bw. Bismass Shillah aliyekuwa kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na baadae kuhamia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) ametangaza kurejea rasmi CHADEMA kwa kile alichodai kuwa amegundua alifanya usaliti kwa kuangalia tamaa yake ya ubunge.
Ameyasema hayo leo Septemba 11, 2025 akieleza kuea kwa sasa hatoama tena CHADEMA na siku akitaka kuondoka chama hicho atakuwa amestaafu siasa.
"nmekosa sana nimetenda makosa ya usaliti kwa viongozi na wanachama nimetambua makosa yangu ni hamu ya kutaka au tamaa ya kutaka kuingia kwenye uchaguzi" amesema Bismass
"nimeamua sitabadilika kwa kuachana na CHADEMA tena nikitoka CHADEMA maana yake nitakuwa nimeacha siasa" ameongeza Bismass
Kabla ya kuhamia CHAUMMA Bismass alikuwa mjumbe mwakilishi mkutano mkuu CHADEMA Taifa na mjumbe WA kamati Tendaji wilaya ya Mkalama. Na alipohamia CHAUMMA alikuwa mtia nia wa kugombea ubunge kwa jimbo la Iramba Mashariki japokuwa alijiondoa CHAUMMA Agosti 12 kabla ya kikao cha mwisho cha kamati kuu cha uteuzi wa wagombea kilichofanyika tarehe 15 Agosti 2025
Chanzo: Jambo Tv