Katika barua rasmi aliyoiwasilisha kwa Katibu wa CHADEMA Wilaya ya Siha, tarehe 24 Juni 2025, Mrisho amesema amekuwa mtumishi mwaminifu wa chama tangu mwaka 1995, akihusika katika kampeni na kushika nyadhifa mbalimbali zikiwemo Diwani na mjumbe wa serikali kwa tiketi ya CHADEMA
“Nimejivunia nafasi hii ambayo niliitumikia kwa uadilifu na mapenzi makubwa bila kujali kulipa gharama zinazotokana na mazingira ya kisiasa nchini,” ameandika Robert Mrisho
Hata hivyo, amesema hali ya kisiasa ndani ya chama hicho imekuwa ngumu, hasa baada ya uchaguzi wa ndani uliofanyika tarehe 3 Oktoba 2024, ambapo licha ya kuchaguliwa tena, amekuwa akikumbwa na mashinikizo na kejeli kutoka kwa makundi ya kisiasa ndani ya chama
“Nimekuwa nikikabiliwa na mashinikizo ya makundi ya uchaguzi ambayo yamekuwa yakinizalilisha kwa maneno ya kejeli, lugha zisizo na stara… hali inayopelekea kushusha heshima yangu binafsi,” amesema kwa masikitiko.
Robert Mrisho alieleza kuwa licha ya kuwa mwanachama wa muda mrefu, mazingira ya sasa ya CHADEMA hayana tena misingi ya demokrasia wala heshima, jambo linalopunguza morali ya kujitolea na kushiriki kikamilifu katika shughuli za chama
Kwa upendo mkubwa, amewashukuru wanachama wa CHADEMA, hasa wa Kata ya Kinua, na wananchi waliompa ushirikiano wakati akiwa Diwani kati ya mwaka 2015 hadi 2020
Kwa sasa bado haijafahamika kama atajiunga na chama kingine cha siasa au kubaki huru, lakini amesisitiza kuwa anaendelea kuwa na dhamira ya kuitumikia jamii yake kwa namna yoyote ile
Chanzo: JAMBO TV