Mkuu,, nafikiri we need to be free.
Nasema hivyo coz kwa sasa ni kama tunachaguliwa watu wa kuwafanya marafiki/maadui na nchi hizi zenye nguvu.
Zikitaka mtu awe gaidi tunakubali, zikitaka mwingine awe shujaa tunakubali pia. Mifano iko mingi. Sisemi kama HAMAS wako sahihi, coz mie siungi mkono mauaji ila hata hao Israel walichofanya huko nyuma hata kupelekea hizi reaction za HAMAS na wanachoendelea kufanya pia sio sawa.
Ila Dunia inalazimishwa iwaone HAMAS ni magaidi kwa sabab wako against na matakwa ya wakubwa. Wangekua pro wakuu wa dunia wangeitwa mashujaa.
Hao wakubwa wanasupport harakati za Taiwan kujitenga na CHINA na kuwa taifa huru lakini hawataki harakati za kuundwa palestina huru.
Walimfurusha Gaddafi kwa sabab ya kuwanyima Raia Uhuru wa demokrasia lakini wanamwacha Theodor Obiang Nguema Mbassogo na Paul Biya waendelee na utawala ktk nchi zao licha ya malalamiko mengi ya ukandamizaji wa demokrasia dhidi yao.
Ni wao ndo walimweka Nelson Mandela kwenye orodha ya magaid na walimuondoa 1998,, sio kwa sabab alikua gaidi then akaacha ila ni kwa sabab alikua against wao lkn alipochukua nchi hakulipiza chochote dhidi ya maslah yao.
So to me, mtu anayeitwa gaidi na hawa wakubwa sio kwa sabab ni gaidi bali ni kwa sabab yuko against them. Na rafiki kwao hata awe na ubaya kiasi gani always atakua shujaa wa dunia.
Kufikia hapo nadhani ipo haja ya kuipitia definition ya "gaidi" kisha kuwa judge watu kama ni magaidi au la kutokana na vitendo vyao vyenye kufanana na definition ya neno gaidi.