Aliyekuwa mgombea Ubunge kupitia Chama cha ACT Wazalendo Jackson Kangoye amejiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakati wa mkutano wa kampenzi za mgombea Urais wa CCM, Samia Suluhu Hassan zilizofanyika Musoma Mjini Oktoba 9, 2025.
Kangoye amesema, watu wanaohamasisha vurugu kipindi hiki cha uchaguzi ni vibaka wanaotaka kuiba mali za watu. Amewataka Watanzania kuimarisha amani iliyoasisiwa na Viongozi waliopita.