No one is ever ready to be a President than a Deputy/Vice President.Karne ya 21 kwanini tuendelee kuongozwa na viongozi wanaoangukiwa na uongozi kama Unabii?
Swadakta kabisa mkuu, na hii ni issue ya kimfumo zaidi kwenye nchi zinazojitambua, ambapo utakuta hapa ndio idara za usalama hufanya kazi kubwa kwa maslahi mapana ya taifa. Na ili kuepusha nchi kuongozwa na mtu ambaye hakutarajia kuwa Rais, endapo Rais aliyepo atashindwa kuendelea na majukumu yake au kufariki, basi watarudi kwenye uchaguzi mkuu. Sijui kwanini Tz hatukurekebisha hii sheria!!!Mimi sikatai, kwa hao wawili kutokuwa tayari kwao kuwa marais; na hasa kwa huyu aliyepo sasa kwenye urais, kwa sababu hakutegemea kabisa kwamba angeshika cheo hicho.
Kwa mtu anayetafuta nafasi kama ya urais, labda tuseme kujiandaa kwake ni kuwa katika siasa na kushika nafasi za ngazi mbalimbali, huku akijijenga atambulike kwa wenzake na wananchi kwa kuwa na misimamo juu ya mambo yanayohusu serikali na nchi kwa ujumla.
Atakuwa ameshika nyadhifa na kufanya maamuzi muhimu juu ya mhimu yanayoihusu nchi.
Kiufupi niseme, mtu huyo atakuwa amejijengea historia inayomtambulisha kwa wenzake na kwa raia.
Mtu huyu pia atakuwa amekwishaonyesha sifa ya kuwa na maono ya nini kifanyike juu ya hatma ya nchi anayotaka kuiongoza.
Haya yote ndiyo yatakayomtambulisha kwa wenzake na wananchi kuwa yeye ni kiongozi na atakapofanya kampeni za uchaguzi atayasisitiza haya, na hatimaye wananchi wanampa ridhaa ya kuwaongoza.
Katika hawa wote tunaowazungumzia hapa, hakuna hata mmoja aliyepitia hatua hizo.
Kwa hiyo tunaweza kusema...Hawakujiandaa.
Wanaojiandaa wanakuwa wabaya sana kwani ni wanasiasa wenye kutegemea kundi kubwa la watu. Huwa wameshatengeneza mgawanyiko kabla hata hawajaapishwa.Magufuli aliupata uRais kwa Zali/hakujiandaa. Samia naye ameupata Urais kwa zali pia, hakujiandaa.
Tuendapo ni Mungu anajua.
Kikwete ni jibu sahihi(?)...; ni kama nauliza huku nikitoa mfano halisi!Wanaojiandaa wanakuwa wabaya sana kwani ni wanasiasa wenye kutegemea kundi kubwa la watu. Huwa wameshatengeneza mgawanyiko kabla hata hawajaapishwa.