Tetesi: Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu akamatwa na TAKUKURU

Status
Not open for further replies.
Nani atamzuia yeye kutumia pesa za umma kujenga kwao? Tz bado sana.
 
Huyu jamaa niliwahi kuambiwa ana mshahara wa zaidi ya 15M.
 
Kiki tu hizo, kiki ikiisha wanamwachia, utasikia hakuna haja ya kuendelea na kesi , tumeona kwa akina Manji na wengine wengi tu
 
Wewe ni kati ya wale ama waliokuwa wamezoea madili na sasa umebanwa au ndg yake na mmoja wa mafisadi wanaonyea ndoo gerezani siyo bure!!
 
Hizo ni siasa nyembamba sana kuhusisha ubomoaji wa bilcanas na kazi kubwa anayofanya mh

Ingekuwa ni siasa nyepesi asingemtuma huyo Mchechu kuvunja bills. Masamaki alikamatwa na mikwara kibao eti fisadi. Leo yuko uraiani anakula upepo mwanana wa bahari. Acheni kick za kishamba.
 
Sasa unazuia ufisadi wa Mchechu, hizo ulizomzuia Mchechu unaenda kununulia wawakilishi wa upinzani. Halafu unatumia hizi hela kurudia uchaguzi!! Kama sio wenda wazimu ni nini?
Mwendawazimu ni yule anayekubali kununuliwa kama ng'ombe! Ama? Tena ni vizuri acha wanunuliwe wote ili siku nyingine wapinzani wajue hasara ya kuokoteza makapi mpaka malaya walioshindikana na kuwapa VIP treatment tena na viongozi top! Unaokoteza mpaka Wema? Kama sio kuishiwa ni nini!
 
Na wale watangazaji wote waliokuwa wanamsifia maisha ni nyumba nao wakamatwe wakaisaidie mahakama kuna vitu watakua wanavijua maana walikuwa wanamwagia sifa kedekede
 
Aende Tanroad !!
Itapendeza sana!
 
Alidhani kusaidia fungu la uchaguzi wa ccm kutamuokoa , laana haiokoleki mjomba .
 
Hakuna Fisadi yeyote atakuwa salama kwenye utawala wa Rais Magufuli. Haiwezekani mamilioni ya watanzania wakose huduma za kijamii wakati viongozi wachache wakinufaika kwa fedha za watanzania.
Tanzania tulichelewa sana kumpata kiongozi kama Rais Magufuli.
 

Sasa kinachowafanya mtembee na kanga moja huku mmeweka vidole juu kwamba mnapambana na rushwa ni nini?
 
Serikalini hakuko salama, maana unaenda kazini basi tu, unaweza kwenda ofisini ukakuta kiti chako kimechukuliwa. Ili uwe na amani kazini lazima ujipendekeze kwa Mkuru nyembe
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…