Siwezi kumuunga mkono rais wa visasi, anayekumbatia mabashite, anayevunja nyumba za wanyonge, anyesigina demokrasia, ameweka kapuni katiba mpya, anayefurahia watu wake kula msoto, asiyetaka wengine waombewe, asiyehudhuria misiba, anayekula rambirambi, anayesema wazi hakuna kuchagua wapinzani kama vile siasa imekuwa uadui, anayezalisha wake za watu, anayehubiri amani wakati kaficha panga mgongoni. Anayetafuta kiki kwa vitu ambavyo ni vya kawaida, nini Msechu, tuliona akina Mramba wakiingia jela. Anayetufanya kwa kutudanganya dollar bilioni moja zimekamatwa, kama vile dollar hizo ni hela ya kukaa kwenye handbag, asiyetimiza ahadi zake, wapi millioni 50 kwa kila kijiji. NIKISEMA NTAMWOMBEA NTAKUWA MNAFIKI KAMA YEYE, AKINILAZIMISHA KUMWOMBEA NTAOMBA KINYUME