TANZIA Aliyekuwa msajili wa Vyama vya michezo nchini, Riziki Majala afariki

TANZIA Aliyekuwa msajili wa Vyama vya michezo nchini, Riziki Majala afariki

Kuna mzee moja yupo hapo Kariakoo na maghorofa yale naye anamuohopa mwanae,anasema huyu mtoto anataka kunitoa roho.
 
Kwa hio dogo kamuua Mzee wake? Mboni story haijakamilika
Aliyekuwa Msajili wa Vyama vya Michezo wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Riziki Juma Majala ameuawa mapema akiwa ndani ya nyumba yake Kibaha kwa Mathias Wilayani Kibaha Mkoani Pwani huku Mtoto wake wa kwanza aitwaye Juma Majala akishikiliwa na Jeshi la Polisi kuhusiana na kifo hicho akidaiwa kuwa amemuua Baba yake kisa kutopewa pesa aliyomuomba Baba yake.


@AyoTV_ imefika nyumbani kwa Riziki Majala Mtaa wa Umwerani na kuongea na Mtoto wa Pili wa Marehemu Majala pamoja na Mashuhuda wengine akiwemo Mjumbe wa Mtaa huo ambapo wamekiri kutokea kwa kifo hicho huku wote wakimnyooshea kidole Mtoto wa kwanza wa Familia kuwa amemuua Baba yake wakisema mara kadhaa amewahi kumpiga na kutishia kumuua Baba yake na kudai hata Mama yake Mlezi aliikimbia nyumba baada ya kutishia kumfanyia vitendo vya ukatili.


Mjumbe wa Mtaa, Salum Abbas Mtowela amesema “ Baada ya kupata taarifa tuliingia ndani tukamkuta Mwanae huyo Juma akatuambia Baba yangu amekufa, tumeongozana na Askari tukakuta mwili juu ya godoro na umefunikwa, kufunua tukaona damu nyingi mdomoni, shingo ni kama ilikabwa na nyuma ya shingo kuna jeraha, kumuhoji Kijana akakiri tuligombana na Baba jana namuomba hela akaninyima baadaye akanipa Tsh. 1500 nikaondoka nimeenda kukesha Bar nimerudi asubuhi namkuta amekufa, akadai hajahusika, huyu Mtoto alipata ajali ya pikipiki kwahiyo kichwa chake kama hakipo vizuri na anavuta bangi hivyo anaongeza tatizo, mwaka jana alitaka kumbaka Mama yake Mlezi Mama akakimbilia kwangu”


Mtoto wa pili wa Marehemu, aitwaye Abdulkarim Majala amesema “Jana sikulala nyumbani nilimuacha Baba na Kaka nyumbani, leo naambiwa nirudi nyumbani kuna msiba, Majirani wanasema Kaka kampiga na kitu kichwani hadi kufariki, Kaka anaweza kuwa kafanya tukio maana ameshawahi kumtishia Baba nitakuja kuua nitakuja kuua, Baba amehamishiwa kutoka BMT akahamishiwa kitengo cha elimu Dodoma ana kama Wiki moja sasa na alipanga kwenda weekend hii Dodoma ili akaripoti”


@AyoTV_ inaendelea na jitihada za kuongea na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani ili kupata taarifa zaidi za kiuchunguzi kuhusu mauaji hayo ya Riziki Majala ambaye ameacha Watoto watatu>> youtu.be/4xBMR_awKvU?si…
 
Rip boss! Mtoto akijaribu kumtishia mzazi siku hiyo hiyo apoteze sifa ya kukaa nae
 
Bangi bangi.
Waswahili wanasema mchelea mwane hulia mwenyewe.
tusipo wakanya watoto wetu waache kuvuta bangi watawauwa.
 
Maisha ya bongo twakutana majukwaanii / ofisini / kwa daladala / sehemu za burdani / mashuleni / vyuoni /nyumba za ibada.... etc
Usimuulize mwenzio walala wapii. Yapo mengi yalojificha nyuma ya maisha ya unayemtizama kwa sasa

RIP
 
Back
Top Bottom