Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Bado haijajulikana alipata wapi ujasiri wa Kuwapangia Watu wengine mambo yao ikiwa yeye hayuko huko, Au mimi ndio sielewi?
Ujumbe wake huu hapa
Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Mkoa wa Singida, Jesca Kishoa Jesca Kishoa amewaomba Wakazi wa Kata ya Gumanga kuwa na imani na Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika 2025 na kuwasisitiza kumchagua Rais Samia kuendelea kuiongoza Tanzania huku akisema anaunga mkono kuwa mwaka 2025 kwa upande wa Urais fomu iwe moja tu ya Rais Samia.
Jesca amesema hayo wakati akiendelea na ziara yake katika Mkoa wa Singida ambapo amesema “Nimekuwa nikisikia Viongozi mbalimbali wa CCM kwa ngazi ya Kitaifa wanasema mwaka 2025 fomu ni moja tu, hayo ni mapendekezo yao na Mimi nataka niseme hapa nikiwa mbele yenu na nyie mtasema kama mnaniunga mkono Kata ya Gumanga Mkalama, tunahitaji fomu moja ya nafasi ya Urais, tunahitaji Mama Samia, CCM ipitishe fomu moja kwa nafasi yake ya Urais na sisi tunaunga mkono”
Jesca Kishoa ametoa pia gesi kwa Wanawake pamoja na jezi za mpira kwa timu mbalimbali ili kutoa hamasa katika Sekta ya Michezo.
PIA SOMA
- Kuelekea 2025 - Wanawake wamchangia Rais Samia Milioni 120 za Fomu ya Urais. Majaliwa aongoza zoezi, asisitiza Fomu ya Urais 2025 itakuwa Moja tu
-Uzi Maalum wa Vibweka na Hekaheka za wanasiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025