Aliyekuwa Mwanajeshi wa KDF, Afikishwa Mahakamani kwa Kuunda Kundi Dhidi ya Uonevu wa Polisi

Aliyekuwa Mwanajeshi wa KDF, Afikishwa Mahakamani kwa Kuunda Kundi Dhidi ya Uonevu wa Polisi

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
977
Reaction score
1,966
Patrick Osoi, aliyewahi kuwa askari wa Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF), alikamatwa Jumanne baada ya kuunda vuguvugu la kupinga ukatili wa polisi pamoja na maafisa wawili wa polisi. Siku ya Jumatano, alifikishwa katika Mahakama ya Kahawa.

Kwa mujibu wa hati ya maombi iliyowasilishwa na Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI), Osoi anadaiwa kuanzisha kundi lililoitwa Fighting Brutality and Impunity (FBI) akiwa pamoja na Jackson Kuria Kimani maarufu kama Cop Shakur na Kimathi Hiram, wakilenga kushirikiana na maafisa waliopo kazini na waliostaafu kupinga maagizo haramu kutoka kwa wakuu wao.

Ujumbe wa Osoi aliouweka katika mtandao wa X (zamani Twitter) ulienea kwa kasi na kupata zaidi ya maoni 400, retweets 900, likes 3,900 na kutazamwa zaidi ya mara 260,000. Kwa mujibu wa DCI, umaarufu huo ulionekana kuwa na uwezo wa kuchochea umma, wakiwemo watu wenye nia mbaya, kushiriki katika matukio yasiyo halali.

Katika machapisho yake, Osoi alionesha nia ya kugombea urais mwaka 2027 kupitia vuguvugu hilo la FBI. Mbali na kazi yake ya awali jeshini, Osoi pia ni mkongwe wa Jeshi la Marekani na anadai kuwa aliwahi kuwa afisa wa Idara ya Ujasusi ya Kitaifa (NIS).

“Kuenea kwa kasi kwa ujumbe huu kunaleta hatari ya kuzuka kwa machafuko, vurugu na uwezekano wa kuratibu vitendo vya fujo wakati uchunguzi bado unaendelea,” ilisomeka sehemu ya hati ya DCI.

Baada ya kukamatwa, Osoi aliwaongoza maafisa hadi kwenye nyumba kadhaa zisizo na watu, zinazodhaniwa kuwa AirBnB zilizopo Nairobi.

Maafisa wa DCI wanaamini kuwa Osoi ana makazi ya siri ambayo amekataa kuyataja kwa hofu kwamba huenda yakawa na ushahidi utakaomhusisha na makosa hayo.

Kwa sababu hiyo, DCI waliomba kibali cha mahakama kufanya upekuzi katika makazi ya Osoi kwa tuhuma za kuwa na silaha na pia wakaomba awekwe rumande katika Kituo cha Polisi cha Muthaiga kwa siku 14 ili uchunguzi ukamilike.

Osoi anatarajiwa kufunguliwa mashtaka ya kujiandaa kutenda kosa la jinai, kumiliki silaha na risasi bila kibali, pamoja na makosa yanayohusiana na uandikishaji na uratibu wa shughuli za ugaidi.

“Makosa yanayochunguzwa ni ya uzito mkubwa na yana adhabu kali endapo atapatikana na hatia. Maombi ya kumuweka rumande si kwa lengo la kumuadhibu, bali kumpa nafasi mpelelezi kukamilisha uchunguzi kwa kina,” linasema andiko la mahakama.
​
==========For English Audience=============​

Patrick Osoi, a former Kenya Defence Forces (KDF) officer who was arrested on Tuesday after forming a movement with two cops with the intention to fight police brutality, was on Wednesday arraigned at the Kahawa Law Courts.According to a notice of motion filed by the Directorate of Criminal Investigations (DCI), Osoi is accused of forming the group called Fighting Brutality and Impunity (FBI) alongside Jackson Kuria Kimani, alias Cop Shakur and Kimathi Hiram, and sought to recruit current and former officers to fight 'illegal orders.'Osoi's post on X went viral, attracting over 400 comments, 900 retweets, 3,900 likes and over 260,000 views.

This, the DCI feared, could mobilise masses, including hostile actors, to engage in unlawful activities.In his posts, the suspect expressed his desire to vie for the presidency in the 2027 elections through the movement. Aside from working in the KDF, Osoi is a United States Army veteran and also claims to be a former National Intelligence Service (NIS) officer."That this viral spread increases the risk of rapid escalation, of unrest, public disorder and coordination of violent acts while investigations are ongoing," read the DCI notice.

Following his arrest, Osoi reportedly took officers to several empty residences believed to be AirBnBs within Nairobi.The DCI sleuths believe that the suspect has a secret residence that he doesn't want to disclose for fear that it may contain evidence that may implicate him. The DCI hence sought a warrant to search Osoi's premises on suspicion of possession of firearms and requested the courts to detain him at Muthaiga Police Station for 14 days.

Osoi is expected to face charges of preparing to commit a felony, possession of a firearm, possession of ammunition without a certificate and offences related to terrorism recruitment and facilitation. "The offence under investigation is serious in nature and carries a severe penalty upon conviction. That the custodial orders sought are not meant to punish the respondent (Osoi) but allow investigators adequate time and thoroughly complete the investigations," added the court document.​
 
Wakenya wanajifanya wajuwaji kumbe mbele ni kiza,.Naona wanajaribu kwa nguvu zote kuifanya nchi yao ifanane hata kidogo na Sudan au Somalia.Nyie zinguaneni na mkija Tanzania tunawakimbiza nyang'au nyie.
 
Hii ingetokea hapa ningejiunga mapema sana
 
Wooooote tunamfahamu huyo mtu endapo hamweki picha !

M-bishi kama huyo hamweki picha ila zawajinga mnaweka
 
Back
Top Bottom