Aaron
JF-Expert Member
- Nov 18, 2010
- 3,019
- 4,693
Nasikiliza taarifa ya habari bbc. Aliyekuwa Naibu Jaji Mkuu wa Kenya leo amekamatwa kwa tuhuma za kifisadi na rushwa...hii haikuwa habari kubwa ila lililonigusa ni haki aliyopewa mtuhumiwa...baada ya kukamatwa alienda kuhojiwa na baadae kufikishwa mahakamani ula muda wa mahakama ulikuwa umeisha hivyo asingeweza kusikilizwa wala kuomba dhamana ila ameachiwa huru kwa kusaini tu baadhi ya masharti.
Sababu za kuachiwa ni kwamba muda wa mahakama ulikuwa umeisha na hivyo hata kama angepata dhamana ya kuweka bondi pesa mabenki yalikuwa tayari yamefungwa hivyo kungezuia haki yake ya kupewa dhamani..hivyo kuachiwa kwa masharti..
Nimejifunza kitu hapa tz mtu anakamatwa mpaka watu waseme apelekwe mahakamani inafikia hatua magereza wanasema hawana gari la kubeba watuhumiwa kupelekwa mahakamani kwa ajili ya dhamani au mambo mengine hivyo watuhumiwa kusota rumande na kunyimwa haki zao za msingi.
Mtu amekamatwa asubuhi kahojiwa mchana na kupelekwa mahakamani pamoja na kuwa muda wa mahakama ulikuwa umeisha lakini amepewa haki yake ya dhamana.. Tujifunze hili watz haki za watu hasa katika mahakama na polisi pale mtu anapokuwa hajatiwa hatiani kwa kosa.
Sent using Jamii Forums mobile app