PreGE2025 Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu CHADEMA Zanzibar apokelewa tena CHADEMA, wakanusha madai ya waliohama Chama

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar kimekanusha madai yaliyotolewa na baadhi ya waliokuwa wanachama na viongozi wa chama hicho, ambao hivi karibuni walitangaza kujiondoa, wakidai kuwa chama hicho kimepoteza mwelekeo na kinakosa stahiki za uendeshaji wa kimamlaka kwa upande wa Zanzibar.

Akikanusha madai hayo mbele ya waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Kanda ya Unguja, Ndugu Hashim Juma, alisema kuwa hakukuwa na stahiki yoyote ambayo chama hicho kilikuwa kinakosa, kwani wanachama walikuwa wakipata stahiki zao kwa mgao sawa. Alieleza kuwa uamuzi wa wanachama hao kujiondoa CHADEMA ni matakwa yao ya kidemokrasia.

Katika hatua nyingine, chama hicho kimempokea aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zanzibar, Hamad Mussa, ambaye alihamia chama cha ACT-Wazalendo na sasa amerejea tena ndani ya CHADEMA. Akiwahutubia waandishi wa habari, Hamad alisema kuwa uamuzi wake wa kurejea ni matakwa yake binafsi ya kidemokrasia.

CHADEMA IMEKOSA VIONGOZI WENYE MAONO
 
Back
Top Bottom