mwakijembe
JF-Expert Member
- Mar 20, 2017
- 1,664
- 2,324
TAKUKURU nao watumbuliwe, hawafanyi kazi yao ya KUZUIA Rushwa, wamekua kama polisi NAO WANASUBIRI WAPELEKEWE AMRI ZA KUCHUNGUZA NA KUPELELEZA.
HII taasisi sijawahi kuelewa majukumu na wajibu wao ni nini. Kwanini isichunguzwe? Rushwa imeongezeka na ipo kila kona, sasa wao wanafanya nini?
Rais ndiye kawa Takukuru na Takukuru ndio wamekuwa RAIS. Yani mpaka rais aseme pale kuna rushwa nendeni mkachunguze, wao primary job yao ni ipi?!
Mpaka Sasa, nishaiona hapa Kuna mupe muruke
Hii issue itapita kimya kimya
Sioni jipya hapo zaidi ya Unafiki na kutaka Kuwafanya Watanzania wote ni Mambumbumbu.
Ova
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu acha tu, halafu hapo wala huyo Kange hachunguzwi bali inafanyika siasa tu ili kuhadaa umma kuwa kuna hatua kwa wezi.
😑🤨😶😐🤔Hivi hili si lilisemwa na Prof.Assad?
Mbwa kala mbwaHuyu mkata mauno ndiyo aliwahi kumchimba biti askari magereza mmoja kwa mbwembwe sasa akipatikana na kesi halafu akatua kwenye gereza analosimamia yule jamaa sijui itakuwaje!
Sent using Jamii Forums mobile app
unaona sasa ,bado haujaelewa, okey ni hivi inakuwaje kangi anatengeneza dili mpaka linaiva na kupakuliwa ilihali usalama wa taifa upo, je hawaezi kutoa taarifa za awali jambo likazuiliwa mapema , inakuwaje watu wanapiga kabisa nyie ndio mstuke, kangi hakupaswa kuchunguzwa na TAKUKURU , lilikuwa ni jukumu la Tiss kumtia hatiani moja kwa moja, huu mzunguko wa sasa umekaa kisiasa zaidi, nadhani utakuwa umenipata japo kidogo misingi ya swali langu,weledi wa hizo idara upi ni :'(bora?)
na wewe umekurupuka, Tiss walipaswa kumchunguza wao na kumzuia asitende aliyotenda,Kangi anapaswa kuchunguzwa na TAKUKURU maana ndio watakao kuja kutoa ushahidi MAHAKAMANI
sio TISS Mkuu.
Ni stori ya kweliNdio. Huoni issue ya makontena ya Makonda haikuchunguzwa wala kuongelewa tena?
Baba hakuamuru mwanae achunguzwe
Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli kabisaMkuu hii stori ni kweli au umetunga?
Hahaha ndio maana wanaenda wanacheka na kurudi wanacheka.Mkuu acha tu, halafu hapo wala huyo Kange hachunguzwi bali inafanyika siasa tu ili kuhadaa umma kuwa kuna hatua kwa wezi.
Presdaa alisema kuuguliwa. Na huyo jamaa me mwenyewe simjui hata kwa sura, ila tunaungaunga dots kutokana na maneno ya kwenye ile hotuba ya mkulu.Ni kuuguza au Msiba?
Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola hivi sasa yupo chini ya ulinzi unaomfanya asiweze kusafiri sehemu yoyote bila Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuwa na taarifa.
Lugola alitenguliwa wadhifa wake baada ya kuhusishwa na mkataba wa kifisadi wa zaidi ya shilingi trilioni 1 wa ununuzi wa vifaa vuya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Hata hivyo, siku chache zilizopita wakati Rais Magufuli akiwaapisha mawaziri na mabalozi aliowateua alikabidhi suala hilo kwa TAKUKURU kwa hatua zaidi na kuisihi mamlaka hiyo kutowaonea huruma waliohusika.
Imeelezwa kuwa maagizo hayo yamekuwa mwiba zaidi kwa Lugola ambaye inaelezwa kuwa kwa sasa anafuatiliwa kwa karibu na vyombo vya usalama.
“Lugola yupo kwenye wakati mgumu sana, kwanza hajui hatma yake, yaani wale aliokuwa akiwapa amri hivi sasa ndiyo wanampa amri na kumchunguza”
“Yupo chini ya ulinzi kila anapokwenda na anachofanya ni lazima kijulikane, yale maisha ya kujimwambafai hayapo tena, sina hakika kama hata vikao vya bunge vilivyoanza jana atashiriki kikamilifu” chanzo kimoja kimelieleza Tanzania Daima.
Hata hivyo imeelezwa kuwa Kangi Lugola hakuonekana jana katika ufunguzi wa vikao vya bunge, jambo lililozua maswali kadhaa, mojawapo likiwa ni kama amekwenda Dodoma au yupo Dar kwa mahojiano na vyombo vya dola.
Siku chache zilizopita Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brig. Jen. John Mbung’o alisema uchunguzi huo umeanza kama sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Rais Magufuli.
Mbung’o alisema wataanza kupata nyaraka zinazohusu mkataba huo na kuhoji kila anayejua na aliyeshiriki katika mchakato wa mkataba huo, ikifuatiwa na kuwahoji watuhumiwa.
Chanzo: Tanzania Daima