Aliyemdhamini CHID BENZ anamuangamiza

Aliyemdhamini CHID BENZ anamuangamiza

Kibo10

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
11,277
Reaction score
8,860
Hatimaye Rapa Chid Benz leo amefanikiwa kupata dhamana na kutolewa rumande na kurejea uraiani.
Kwa masikitiko makubwa kabisa na dhubutu kusema anaye mmaliza na kumfuta chid benz kwenye ramani ya music au hata maisha yake ni huyo aliyeenda kumwekea dhamana.

Kama alikuwa anasikia kupitia watu kuwa Chid ni teja kitendo kile cha kudakwa live air port kulidhibitisha na kufuta ubishi wa miaka mingi ni kwa nini asingemwacha rumande ili apate muda wa kupumzisha damu then akitoka gerezani moja kwa moja akapatiwe matibabu?

Kwa upande wangu naona huyo aliyemwekea dhamana ni kama amemkatia tiketi ya kifo tu wala sioni msaada wake!

Ni hayo tuu.
 
Kwa nini ateseke jela?? Wakati hata huko jela hayo madawa yanapatikana!! Bora aje ajidungie uswahilini ale na Chips Yai

Nashangaaaa.....
Wakati my friend walimdanja na akawa tunampelekea "Serengeti baridiiii" kila siku.
Jela mbaya ukiwa huna hela tu.....
Kama unayo hao mabwana jela unawaita wachumba tu.
 
Chid Benz madawa yamemuharibu sana,la sivyo angekuwa mbali sana .Wauza unga wote natamani wafe kwa ebola

Wakafie huko wanakaoenda kubeba mizigo wasije wakafia huku nchini wakatuambukiza buree.....lol
 
Kwa nini ateseke jela?? Wakati hata huko jela hayo madawa yanapatikana!! Bora aje ajidungie uswahilini ale na Chips Yai

Tofauti ni kwamba kule jela hawezi kupata kwa kiwango kikubwa au kwa urahisi kama huku uraiani
Nakuakikishia kitendo cha kumdhamini leo leo leo anaingia maskani kujidunga ni upuuzi
 
Nashangaaaa.....
Wakati my friend walimdanja na akawa tunampelekea "Serengeti baridiiii" kila siku.
Jela mbaya ukiwa huna hela tu.....
Kama unayo hao mabwana jela unawaita wachumba tu.
unapajua jelaaaaa:cool2:
 
Hatimaye Rapa Chid Benz leo amefanikiwa kupata dhamana na kutolewa rumande na kurejea uraiani.
Kwa masikitiko makubwa kabisa na dhubutu kusema anaye mmaliza na kumfuta chid benz kwenye ramani ya music au hata maisha yake ni huyo aliyeenda kumwekea dhamana.
Kama alikuwa anasikia kupitia watu kuwa Chid ni teja kitendo kile cha kudakwa live air port kulidhibitisha na kufuta ubishi wa miaka mingi ni kwa nini asingemwacha rumande ili apate muda wa kupumzisha damu then akitoka gerezani moja kwa moja akapatiwe matibabu?
Kwa upande wangu naona huyo aliyemwekea dhamana ni kama amemkatia tiket ya kifo tu wala sioni msaada wake!
Ni hayo tuu...!!!!!!!

Wewe ulikuwa unatakaje?ulitaka aendelee kukaa selo?
 
Kwa nini ateseke jela?? Wakati hata huko jela hayo madawa yanapatikana!! Bora aje ajidungie uswahilini ale na Chips Yai

Ni Kweli kabisa hata jela madawa na bangi vinapatikana watu hawaelewi hilo bora ajidunge mtaan huku anapata chakula kizuri!!
 
Kakuambia nani rumande kunasafisha damu ya teja.??

Angekufa ghafla.

Mshukuru aliomwekea dhamana.,, anaweza anza matibabu.

Ana somo la kujifunza sasa.
 
Tatizo lako unafikiri rumande kuna tibu kila kitu! Mtu mwenye tatizo la kutumia madawa ya kulevya rumande hakumfai labda kama unataka afie huko!

Chid Benz ana hitaji msaada wa matibabu na kisaikolojia na ana hitaji msaada kabisa!
 
Chid Benz madawa yamemuharibu sana,la sivyo angekuwa mbali sana .Wauza unga wote natamani wafe kwa ebola

Huyu jamaa ana kipaji cha ajabu sana bhasi tu alijiingiza kwenye mambo yasiyo faa!
 
Back
Top Bottom