Aliyemkaba Tambwe apewa red card tena

Lupweko

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2009
Posts
23,566
Reaction score
24,891
Yule mchezaji wa Ruvu Shooting, George Michael, ambaye wiki kadhaa zilizopita alifungiwa na TFF kucheza mechi tatu kwa kosa la kumkaba koo na kumnyanyasa mshambuliaji wa Yanga, Amis Tambwe, leo hii amepewa kadi nyekundu wakati timu yake ya Ruvu ilipokuwa ikicheza na Polisi Morogoro. Mchezaji huyo alilimwa kadi hiyo dakika ya 60 ya mchezo baada ya kumpiga kwa kiwiko mchezaji mmoja wa Polisi Moro. Timu hizo zimetoka sare ya 0-0 huku ikiwa ndio mechi ya kwanza kwa George Michael baada ya kumaliza adhabu ya kukosa mechi tatu

Mchezaji huyo atalazimika kuzikosa mechi nyingine mbili za ligi ili kutumikia adhabu ya kupewa straight red card na hivyo kumfanya kukosa mechi tano kwa adhabu tu hadi sasa.
 
Mchezaji mpumbavu sana huyo..ni aina ya wachezaji tulionao nchi hii hana tofaut na mchezaji kiungo mmoja wa Simba anaitwa Banda
 
Banda mtalala na kuweweseka jina lake. Kwani ndio aliyewakata ngebe na hao walinzi wenu walizoea kucheza kibabe.
 
Banda mtalala na kuweweseka jina lake. Kwani ndio aliyewakata ngebe na hao walinzi wenu walizoea kucheza kibabe.

Acha uzembe ww..mambo ya kizaman hayo..kupiga madole watu,kupiga vipepsi au kurudisha pale ambapo umetendewa madhambi sio ujanja ndo mana soka letu haliwez kuendelea...katika muda huu ambao kamera za Azam zinaonesha matendo mengi viwanjan ni mpumbavu pekeee ndio ataendekeza huo ujinga...that is not sportmanship
 
Mzembe wewe una uchungu wa kufungwa. Kuna wanaocheza kibabe kama Haroub Cannavaro na Kelvin Yondani. Kupiga vipepsi,kusukuma na kucheza rafu mbaya.Mechi ya jumapili Cannavaro alimsukuma refa baada ya kucheza rafu ya kijinga na kuonyeshwa kadi ya njano. Angekuwa refa makini angekula nyekundu.Ulitaka Banda avumilie huo ujinga ndio umuone mstaarabu. Wacha kujificha kwenye kupenda haki kwani mapenzi ya timu yako yamekuumbua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…