Lupweko
JF-Expert Member
- Mar 26, 2009
- 23,566
- 24,891
Yule mchezaji wa Ruvu Shooting, George Michael, ambaye wiki kadhaa zilizopita alifungiwa na TFF kucheza mechi tatu kwa kosa la kumkaba koo na kumnyanyasa mshambuliaji wa Yanga, Amis Tambwe, leo hii amepewa kadi nyekundu wakati timu yake ya Ruvu ilipokuwa ikicheza na Polisi Morogoro. Mchezaji huyo alilimwa kadi hiyo dakika ya 60 ya mchezo baada ya kumpiga kwa kiwiko mchezaji mmoja wa Polisi Moro. Timu hizo zimetoka sare ya 0-0 huku ikiwa ndio mechi ya kwanza kwa George Michael baada ya kumaliza adhabu ya kukosa mechi tatu
Mchezaji huyo atalazimika kuzikosa mechi nyingine mbili za ligi ili kutumikia adhabu ya kupewa straight red card na hivyo kumfanya kukosa mechi tano kwa adhabu tu hadi sasa.
Mchezaji huyo atalazimika kuzikosa mechi nyingine mbili za ligi ili kutumikia adhabu ya kupewa straight red card na hivyo kumfanya kukosa mechi tano kwa adhabu tu hadi sasa.