Aliyemnywesha tembo bia mbugani achunguzwa na mamlaka za Kenya

Aliyemnywesha tembo bia mbugani achunguzwa na mamlaka za Kenya

McLaren

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2025
Posts
1,170
Reaction score
3,743
Mamlaka za wanyamapori nchini Kenya zimeanzisha uchunguzi baada ya video za mtalii wa Kihispania kusambaa mtandaoni zikimuonyesha akimimina bia kwenye mwembe wa ndovu. Tukio hilo lililofanyika katika hifadhi binafsi ya Ol Jogi Conservancy, Kaunti ya Laikipia, limezua hasira kubwa kwenye mitandao ya kijamii.

Katika video hiyo, mtalii huyo anayejulikana mtandaoni kwa jina la Skydive_Kenya alionekana akinywa bia ya Tusker kisha kumpa iliyosalia ndovu anayejulikana kama Bupa. Ndovu huyo maarufu, mwenye pembe moja iliyoharibika, aliokolewa mwaka 1989 kutoka mauaji ya halaiki ya ndovu nchini Zimbabwe na kupelekwa Ol Jogi akiwa na umri wa miaka minane.

Uongozi wa Ol Jogi umelaani kitendo hicho na kueleza kuwa ni “hatari, kinyume na maadili yao na hakiwezi kuvumiliwa.” Walisema wanachukulia tukio hilo kwa uzito mkubwa na wamesisitiza dhamira yao ya kulinda heshima na ustawi wa wanyama walioko chini ya uangalizi wao.

Msemaji wa Shirika la Huduma za Wanyamapori Kenya (KWS), Paul Udoto, amethibitisha kuwa uchunguzi unaendelea.

Aidha, Dylan Habil kutoka Ol Pejeta Conservancy amekosoa mtalii huyo kwa kukiuka kanuni zao baada ya video nyingine kuonyesha akiwalisha faru kwa karoti. “Hawa si wanyama wa kufugwa, na wageni hawaruhusiwi kuwapapasa,” alisema.

elephant.png


======================================

Several investigations have been launched after a Spanish man in Kenya posted videos of himself pouring beer down an elephant's trunk - sparking anger on social media.

He was filmed in a wildlife reservation drinking from a can of Tusker, a popular local beer, before giving the rest of it to the elephant.

"Just a tusker with a tusked friend," he captioned one clip posted on Instagram, which was later deleted from his account after a backlash from Kenyans in the comments.

The landscape and a well-known bull elephant pointed to it being filmed at the Ol Jogi Conservancy in the central county of Laikipia. Ol Jogi Conservancy has since been in touch to confirm the incident occurred last year at the privately owned wildlife sanctuary - saying it was "unacceptable, dangerous and completely against our values".

Earlier a member of the staff there had told the BBC he was shocked by the behaviour of the yet-to-be identified guest.

Source: BBC News
 
Aliyesema tembo hua hawanywi pombe nani tembo mwenyewe alimanusra acheni ainjoy
 
Too much ado about nothing. Probably Jumbo enjoyed the shared drink.
 
Pombe yenyewe ni Tembo,hapo Tembo kapewa Tembo.
 
Nyani hawawezi kumfanya chochote huyo binadamu(Mzungu)
 
Back
Top Bottom