Aliyemshambulia binti kwa fimbo Katoro atiwa mbaroni

Aliyemshambulia binti kwa fimbo Katoro atiwa mbaroni

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
446
Reaction score
1,113
Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linamshikilia Jackline Peter, mkazi wa Mji
Mdogo wa Katoro, Wilaya na Mkoa wa Geita, kwa tuhuma za kumshambulia kwa kutumia fimbo Rahel Jumanne, aliyemtuhumu kumwibia fedha zake.

Tukio hilo la kikatili lilitokea Agosti 26 2026, majira ya saa 5.00 asubuhi, nyumbani kwa mtuhumiwa Jackline Peter baada ya kudai ameibiwa fedha kiasi cha Shilingi 60,000/= zilizokuwa kwenye pochi chumbani kwake na kuanza kumtilia shaka Rahel Jumanne aliyekuwa amemtembelea kwake.

Siku ya tukio, baada ya fedha hizo kudaiwa kupotea, mtuhumiwa alimkamata
mwathirika na kuanza kumshambulia kwa fimbo. Wakati vitendo hivyo vya ukatili vikiendelea, mfanyakazi wa kazi za ndani wa mtuhumiwa alielekezwa kurekodi tukio hilo kwa kutumia simu ya mtuhumiwa na baadaye mtuhumiwa kusambaza picha mjongeo hiyo kwenye mitandao ya kijamii.

Baada ya Jeshi la Polisi kubaini tukio hilo kwenye mitandao ya kijamii, lilianza ufuatiliaji wa mara moja na kufanikiwa kubaini eneo la tukio, kumtambua mtuhumiwa na kumkamata, ambapo kwa sasa anaendelea kuhojiwa.

Jeshi la Polisi linakamilisha uchunguzi wa tukio hilo na mara baada ya kukamilika, mtuhumiwa atafikishwa katika mamlaka husika za kisheria kwa hatua zaidi.

1788158072553.png
 
Mtuhumiwa afikishwe Mahakamani na kuhukumiwa kwa mujibu wa sheria kama atakutwa na hatia,
Hii ni habari njema.
 
Nipo mjini katoro ngoja nitafute wenyeji wanipeleke kwa huyo mtuhumuwa nikamdodose.
 
Back
Top Bottom