Aliyemtupa mtoto Nzega Tabora bado hajajulikana alipo. Jeshi La Polisi bado linamtafuta

Aliyemtupa mtoto Nzega Tabora bado hajajulikana alipo. Jeshi La Polisi bado linamtafuta

McLaren

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2025
Posts
1,170
Reaction score
3,743
Wakuu,

Hali ya mtoto mchanga aliyetelekezwa kwenye nyumba ya kulala wageni sakafuni eneo la mapokezi wilaya ya Nzega mkoani Tabora akiwa na siku tano baada ya kuzaliwa inaendelea vizuri huku akiwa chini ya uangalizi madaktari katika hospitali ya wilaya ya mji wa Nzega. Mama wa mtoto huyo bado hajajulikana alipo

Mtoto huyo mchanga wa siku tano baada ya kutelekezwa takribani mwezi mmoja uliopita na mwanamke anayedhaniwa kuwa ni mama yake mzazi kwenye nyumba ya kulala wageni na kisha mwanamke huyo kutokomea kusikojulikana alipatiwa hifadhi katika hospitali ya mji wa Nzega na kuzawadiwa jina la Grace Samia Suluhu Hassan.


 
Back
Top Bottom